Thursday , 23 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Meya wa jiji atoa siku 12 kwa wakwepa kodi
Habari za Siasa

Meya wa jiji atoa siku 12 kwa wakwepa kodi

Mwita Isaya, Meya wa Jiji la Dar es Salaam (aliyesimama) akizungumza na wafanyabishara wa stendi ya Ubungo
Spread the love

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Issaya Mwita ametoa siku 12 kwa wafanyabiashara wasiolipa kodi katika Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo kuhakikisha wanalipa vinginevyo atawachukulia hatua kali, anaandika, Jovina Patrick.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, alipofanya ziara ya kushtukiza akiwa ameambatana na Kamati ya Uongozi na Fedha ya Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na wafanyabiashara hao, Mwita amesema kuwa wasipolipa kodi hiyo ifikapo Agosti hatua kali juu dhidi yao zitachukuliwa kwani baadhi yao kuna wadaiwa sugu.

Anasema “Na itakapofika mwezi wa nane nitaagiza wasaidizi wangu na yeyote atakayekuwa hajalipa kodi hatua kali zichukuliwe juu yake”.

Meya amewaonya wafanyabiashara hao juu ya ukaidi wao kutolipa kodi na kusema kuongeza kuwa fedha wanazolipa ni kwa ajili ya manufaa yao wenyewe .

“Pesa hiyo mnayolipa ndiyo inayonunulia umeme, kulipia maji, usafi wa vyoo ni wajibu wenu kulipa kodi,” amesema Meya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!