Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi wazidi kuwahenyesha wapinzani
Habari za SiasaTangulizi

Polisi wazidi kuwahenyesha wapinzani

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Kunti Majala kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma
Spread the love

HALI ya kisiasa kwa vyama vya upinzani nchini inazidi kuwa mbaya kutoka na makada wa vyama hivyo kuendelea kukamatwa na kuswekwa rumande na kunyimwa dhamana zaidi ya saa 48 za kisheria bila ya kupelekwa mahakamani, anaandika Dany Tibason.

Wabunge wengi wa upinzani pamoja na wanachama na wafuasi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara kwa amri ya wakuu wa mikoa na wilaya kwa madai ya kufanya mikusanyiko isiyokuwa na vibali.

Wimbi hilo limezidi kuendelea baada ya jana Mbunge wa Viti Maalum, Kunti Majala amekamatwa na kuhojiwa kwa zaidi ya saa 3 kwa madai ya kufanya mkutano wa hadhara kijiji cha Mapango kata ya Chadama Wilaya ya Chemba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema kulikuwa na malalamiko kuwa mbunge huyo alikuwa anatukana serikali na kutoa lugha za kuudhi.

“Kwa kuwa sisi ndiyo tunatoa vibali na mwenyewe hana kibali kwenye maeneo hayo anayokwenda kwenda kwa hiyo OCD akachukua hatua ya kuanza kufuatilia kwa sababu ilikuwa inaanza kuleta uvunjifu wa amani,”amesema Mambosasa.

Mambosasa amesema mbunge huyo anatakiwa kuomba kibali cha mikutano yake ili wajue kuwa kama ni inafanyika wapi na itakuwa ndani au nje, maana wanatakiwa kufanya mikutano ya ndani pekee.

Kwa upande wake, Kunti amesema Katibu wa Chadema Wilaya ya Chemba aliandika barua kwa OCD wa wilaya hiyo akieleza kuwa atafanya (Kunti) ziara katika jimbo hilo kuanzia Julai 17 hadi 20 mwaka huu.

Amesema Julai 16, katibu wa jimbo amepokea simu kutoka kwa OCD akimuuliza kuwa ofisi za chama hicho ziko eneo gani.

“Katibu alimweleza kuwa ofisi zipo Mrijo na akamweleza kuwa mikutano yao imeruhusiwa lakini wasishiriki watu wan je ya wilaya hiyo na kwamba lugha ziwe za staha,” amesema Kunti.

Hata hivyo, amesema akiwa katika kijiji cha Mapanga saa 9.45 jioni kwenye mkutano wa hadhara alikuja polisi na kumueleza kuwa OCD anashida na yeye na kumtaka kwenda kituoni.

Amesema mara baada ya mkutano kumalizika alikwenda katika kituo cha polisi na kutakiwa kuandika maelezo kwanini amefanya mkusanyiko usio halali.

“Baada ya kuandika maelezo waliniruhusu kuondoka na niripoti tena kituoni Julai 19 mwaka huu. Hata hivyo wakati tunatoka aliuliza viongozi wa wilaya wako wapi kuna barua anataka kuwapatia,” amesema.

Amesema baada ya viongozi wa wilaya chama kuchukua barua hiyo na kuifungua walikuta ziara hiyo imezuiwa.

Hata hivyo amesema ni jambo la kushangaza kuona viongozi wa kisiasa wa chama tawala wanaendelea kufanya mikutano tena kwa kutumia vyombo vya habari na wakati mwingine kufanya mikusanyiko na wao wanaonekana kuwa sawa lakini inapofanyika kwa viongozi wa kisiasa wa upande wa upinzani wanapata nisukosuko na kutiwa ndani bila kuwa na sababu ya msingi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!