Saturday , 9 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Membe arudisha kadi ya CCM, mamia wamsindikiza
Habari za SiasaTangulizi

Membe arudisha kadi ya CCM, mamia wamsindikiza

Spread the love

BERNARD Kamillius Membe, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, ametangaza kurejesha kadi yake ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Membe amerejesha kadi hiyo leo Jumatatu tarehe 6 Julai 2020 nyumbani kwake Rondo mkoani Lindi.

“Leo saa 6 na nusu mchana mimi na mke wangu nikisindikizwa na mamia ya wananchi wa Rondo, tumerejesha kadi zetu za CCM kwa wenyewe.”

“Nimemwandikia KM (katibu mkuu) wa CCM kuhusu tukio hilo na kukishukuru chama kwa mema yote kilichonitendea. Nawatakia kila la heri viongozi na wanachama wote,” ameandika Membe.

Tarehe 28 Februari 2020, Kamati Kuu ya CCM ilitangaza kumfukuzwa uanachama Membe kwa madai amekuwa akikiuka taratibu na miongozo ya chama hicho tangu mwaka 2014.

Tarehe 13 Desemba 2019, Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana jijini Mwanza chini ya Mwenyekiti wake, Rais John Pombe Magufuli ilitoa maagizo kamati ya maadili kuwahoji Membe na makatibu wakuu wastaafu wa CCM,  Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba.

          Soma zaidi:-

Wakati halmashauri kuu ilitoa maagizo hayo, ililidhia msamaha uliokuwa umekwisha kutolewa na Rais Magufuli dhidi ya wabunge wake watatu, William Ngeleja (Sengerema), Nape Nnauye (Mtama) na January Makamba (Bumbuli).

Msingi wa mahojiano hayo ya sauti zao, yalitanguliwa na waraka wa Kinana na Makamba kuandika tarehe 14 Julai 2019 kwenda kwa Katibu wa Baraza la Wazee la CCM, Pius Msekwa wakidai uongozi hauwalindi dhidi ya mtu ambaye alikuwa akiwadhalilisha na walimwelezea analindwa na mtu mwenye mamlaka.

Waraka huo, ulifuatiwa na sauti za wanachama hao wasambaa mitandaoni wakizungumzia kuporomoka kwa uongozi wa CCM akiwemo Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!