Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe aweka ‘sharti’ la Lowassa 2015
Habari za SiasaTangulizi

Membe aweka ‘sharti’ la Lowassa 2015

Spread the love

BERNALD Membe, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Awamu ya Nne, anataka kile alichofanyiwa Edward Lowassa mwaka 2015, afanyiwe sasa. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, ili agombee urais kupitia vyama vya upinzani, basi wapinzani waungane na kumpa fursa hiyo.

Hiki ndicho kilichofanyika katika uchaguzi mkuu 2015, baada ya vyama vya vinne vya upinzani kumpa fursa Lowassa aliyetoka CCM na kujiunga nao kugombea urais.

       Soma zaidi:-

Alitoka CCM baada ya jina lake kukatwa katika mbio za urais ndani ya CCM akiwa miongoni mwa wanachama 42 waliojitosa kumrithi Rais aliyekuwa anamaliza muda wake, Jakaya Mrisho Kikwete.

Vyama hivyo vilivyoshirikiana na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vilikuwa ni Chadema, NLD, CUF na NCCR-Mageuzi.

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo akibadilishana mawazo ya Bernard Membe, Waziri wa zamani Mambo ya Nje Tanzania

Alipoulizwa na mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Sammy Awami kwamba yupo tayari kugombea kupitia upinzani, Membe alijibu “iwapo nitaombwa” akisitiza ili afanye hivyo, basi ni muhimu vyama vya upinzani vikaungana.

Lowassa alijiengua CCM na kujiunga upinzani baada ya kukosa nafasi ya kugombea urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015.

Hata hivyo, tarehe 1 Machi 2019, Lowassa aliyewahi kuwa waziri mkuu alitangaza kurejea CCM na kupokelewa na Rais John Magufuli ofisi ndogo za chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!