Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee, wenzake wamvaa Mwigulu sheria ya manunuzi ikisubiri kupitishwa
Habari za Siasa

Mdee, wenzake wamvaa Mwigulu sheria ya manunuzi ikisubiri kupitishwa

Halima Mdee
Spread the love

WAKATI muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya 23, ikisubiri kupitishwa bungeni jijini Dodoma, baadhi ya wabunge wamedai bila Serikali kuweka mikakati ya ufuatiliaji na usimamizi  watekelezaji wake, haitsaidia katika kutokomeza vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Maoni hayo yametolewa leo tarehe 7 Septemba 2023, bungeni jijini Dodoma, wakichangia mjadala wa muswada huo unaolenga kufuta Sheria ya Ununuzi ya Umma Na. 7 ya 2011.

Mbunge Viti Maalum, Halima Mdee amesema changamoto ya ubadhirifu wa fedha za umma unaotokea katika manunuzi na ugavi mbalimbali, inatokana na baadhi ya watumishi wa Serikali kutokuwa na weledi, hivyo mabadiliko ya sheria hiyo yanapaswa kwenda sambamba na mikakati ya usimamizi na ufautiliaji wa suala hilo.

“Changamoto kubwa tuliyonayo ni kuwa na watu wenye uweledi, watu wenye uzalendo wanaopenda taifa lao na kutekeleza wajibu waliopewa kuutekeleza kisheria,” amesema Mdee.

Katika hatua nyingine, Mdee alishauri mamlaka ya waziri wa fedha kutunga kanuni za manunuzi ya umma yapunguzwe, badala yake kanuni hizo zitungwe au ziidhinishwe na mhimili huo kabla hazijatumiwa.

“Haiwezekani Bunge likaruhusu waziri apewe mamlaka makubwa namna hiyo, kwa mujibu wa kanuni ya 128, maeneo 28 muhimu amepewa waziri akatunge kanuni. Hii haiwezekani vinginevyo tukubali akitunga sheria kanuni alete kwenye kamati ya Bunge ya bajeti na sheria ndogo, kabla hazijafanya kazi,” amesema Mdee.

Mbunge wa Handeni Mjini, Kwagilwa Nhamanilo, alishauri Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), iimarishwe ili iweze kusimamia mikataba ya manunuzi ambayo taasisi za umma zinaingia na sekta binafsi, kwa lengo kulinda maslahi ya nchi.

“Tukiangalia wajibu, usimamizi na utekelezaji wa mikataba ni vyema kuiwezesha ofisi ya AG sababu sheria ya manunuzi haikamiliki bila kuwa na mikataba. Lazima tuiwezeshe kibaje, kusomesha watalaamu wetu na kusimamia kwa ukaribu sisi kama Bunge,” amesema Nhamanilo.

Naye Mbunge wa kuteuliwa, Shamsi Vuai Nahodha amesema “nchi yetu inatumia zaidi ya asilimia 70 ya fedha za bajeti katika masuala ya manunuzi na ugavi, hiki ni kiwango kikubwa sana kwa mantiki hiyo tuna wajibu kutunga sheria madhubuti ili tuweze kudhibiti vitendo vya rushwa na ukosefu wa maadili.”

“Lakini suala la kuwa na sheria nzuri ni jambo moja na suala la kuwa na sheria inayotekelezeka ni jambo jingine. Ili tuweze kusimamia sheria hii ipasavyo ninapednekeza Seriali kuweka watendaji walio makini,” amesema Nahodha.

Awali akisoma kwa mara ya pili muswada huo, Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, alisema unalenga kuweka masharti bora ya usimamizi wa manunuzi ya umma na ugavi na uondoshaji mali kwa njia ya zabu.

Pia, sheria hiyo pendekezwa inalenda kutatua changamoto zilizobainika katika utekelezaji wa mashari na utaratibu wa maunusiz, ikiwemo kutokutofautisha masharti ya ununuzi kati ya taasisi za umma, kutojumisha masuala ya ugavi, kutokuwa na sehemu mahususi inayoanisha masuala ya usimamizi wa mikataba ya manunuzi kwa njia ya kielktroni na ukomo wa thamani ya mradi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!