Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu afufua matukio ya wasiojulikana, ambana Rais Samia
Habari za SiasaTangulizi

Lissu afufua matukio ya wasiojulikana, ambana Rais Samia

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (Chadema) Bara, Tundu Lissu, amedai bila ya wahanga wa vitendo vya watu wasiojulikana kupatiwa haki zao, falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuhusu upatanisho, haitawezekana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Lissu ametoa kauli hiyo leo tarehe 7 Septemba 2023, katika mkutano wa hadhara  uliofanyika Kata ya Issenye mkoani Mara, wakati akikumbushia miaka sita tangu alipojeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana, jijini Dodoma.

“Watu walioumizwa kipindi hicho kwa namna mbalimbali ni wengi sana, wapo waliopoteza ndugu zao wanadai majibu kwa nini ndugu zao waliuawa, wapo waliopotezwa miaka mitano sasa haijulikana wamepelekwa wapi na ndugu zao wanataka wajue waliowapoteza wapo wapi,” amesema Lissu.

Mwanasiasa huyo amesema “rais wetu anazungumzia upatanishi, hakuna upatanishi bila ukweli, bila kutuambia nani aliyekosa na kwa nini alikosa, aliyekosew anarekebishwaje. Upatanishi sio maneno lazima uendane na vitendo. Ili kupata upatanishi lazima waliotyukosea wajulikane, watubu dhambi na waliosewa wafutwe machozi yao.”

Akizungumzia tukio la kushambuliwa kwa risasi na wasiojulikana lililotokea tarehe kama ya leo 2017, Lissu amemhoji Rais Samia na Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura, wana mpango gani wa kuwachukulia hatua waliolitekeleza.

“Rais Samia alikuwa makamu wa Rais wakati ule na sasa ni rais, atuambie nani aliyekuja kuniua tarehe kama ya leo miaka sita iliyopita na ana mpango gani wa kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria aliyoapa kuilinda na kuitekeleza,” amesema Lissu na kuongeza:

“La pili aniambie angalau ana mpango gani kwa sababu niliumizwa nikiwa bungeni na mbunge ana haki ya kutibiwa kwa gharama ya serikali. Mama aniambie ana mpango gani kama upo wa kulipa stahili zote za matibabu kwa mujibu wa sheria.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!