Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari Mdee wenzake saba waitwa mahakamani kuhojiwa
HabariSiasaTangulizi

Mdee wenzake saba waitwa mahakamani kuhojiwa

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa amri ya wito kwa Halima Mdee na wenzake saba kufika mahakamani hapo Tarehe 26 Agosti 2022 ,kwa ajili ya kuhojiwa na Mawakili wa Chadema. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea)

Leo tarehe 29 Julai 2022, Jopo la Mawakili wa Chadema liliongozwa na Peter Kibatala mbele ya Jaji Cyprian Mkeha wameiomba Mahakama hiyo Mdee na wenzake kufika mahakamani hapo ili upande huo uwahoji.

Mbali na Mdee wengine walioitwa ni pamoja na Jesca Kishoa, Grace Tendega, Hawa Mwaifunga, Nusrat Henje, Cecil Pareso, Ester Matiko na Ester Bulaya.

Jaji Mkeha ametoa amri ya wanasiasa hao kufika mahakamani siku hiyo.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Kibatala ameeleza kuwa sehemu ya mahojiano watakayoyafanya na waombaji hao kuhusu yale waliyoyaeleza kwenye kiapo chao.

Ameeleza kuwa kwenye kiapo cha wanasiasa hao wameeleza kuwa Chadema kimewateua kihalili kwenda bungeni ambapo upande huo utahoji uhalali wao.

Mbali na ombi hilo tarehe 5 Agosti Mawakili wa Chadema watawasilisha kiapo kinzani dhidi ya kiapo cha waombaji.

Mdee na wenzake wanapinga kufutiwa uanachama wa chama hicho na kuiomba mahakama kupitia mchakato wa kutimuliwa kwao.

Pamoja na kupinga mchakato wameomba mahakamani hapo Chadema iwape haki ya kuwasikiliza, kutengua uamuzi wa baraza kuu wa kufukuzwa chamani.

Uamuzi wa Kamati Kuu uliwafanya Mdee na wenzeke kukata rufaa iliyosikilizwa tarehe 12 Mei 2022 na Baraza Kuu la Chama hicho na kupelekea kufukuzwa uanachama wao.

Kwenye kesi hiyo wanasiasa hao 19 wanawakilishwa na jopo la mawakili lililoongozwa na Ipioinga Panya, Edson Kilatu, Emmanuel Ukashu, na Aliko Mwamanenge.

Mdee na wenzake wanawashtaki Bodi ya Wadhamini ya Chadema kwa niaba ya Chama hicho, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Taifa (NEC).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

BiasharaTangulizi

TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari

Spread the love  CHAMA cha wanasheria Tanzania (TLS), kimejitosa katika sakata la...

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

error: Content is protected !!