August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali: Nyongeza mishahara imelenga wengi wenye mishahara ya chini

Spread the love

SERIKALI imesema nyongeza ya kima cha chini cha asilimia 23.3 kinanuafaisha asilimia 75 hadi 78 ya watumishi ambao wana mihahara midogo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Amesema malalamiko mengi yanafanywa na wale wenye mishahara mikubwa ambao ni asilimia 22 tu watumishi.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa tarehe 29, Julai, 2022 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu nyongeza ya mishahara ilianza kutolewa Julai mwaka huu.

“Kama nilivyosema sisi sote ni watumishi iwe sekta ya umma au binafsi, kwahiyo ni jambo letu pamoja , nataka niwaambie lengo la kuwalenga wafanyakazi wetu wa chini ni kwasababu kundi kubwa ndiyo limenufaika na asilimia 23.3 na inaenda kidogo hadi asilimia 75 hadi asilimia 78,” amesema Majaliwa.

“Na hawa wanaolalamika wameongeza Sh 20,000 wapo kwenye hii asilimia 22 na ndiyo unawakuta mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi, mameneja ambao na wao kidogo wana mshahara unaotosha ni asilimia 22 tu na ndiyo wameweza kupaza salionekane jambo kubwa,” amesema.

Akitolea mfano wa mawaziri, Majaliwa amesema mawaziri wamepata asilimia 0.7 “sasa wanayopata hiyo ni wale wenye kipato kikubwa na nyongeza yake ni ile ambayo inatamkwa tamkwa.

Amesema asilimia 23 iliyotajwa haijalipa watu wote ni kutokan ana ile fomula ilitamkwa kwamba itaongeza viwango vya mishahara ambao wanaonufaika ni wa viwango vya chini ambao ni hawa asilimia 75 hadi asilimia 78 ya watumishi.

error: Content is protected !!