Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge viti maalumu CCM aapishwa
Habari za Siasa

Mbunge viti maalumu CCM aapishwa

Spread the love

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson leo tarehe 13 Septemba, 2022 amemuapisha Tamima Haji Abass kuwa mbunge wa Bunge hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tamima amekula kiapo hicho akichukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum, Irene Ndyamkama aliyefariki dunia April 24,2022.

Kwa mujibu wa taratibu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatakiwa kupeleka jina la mtu kutoka ndani ya chama husika kuziba nafasi ya mbunge huyo aliyefariki.

Iwapo kama marehemu angekuwa mbunge wa kuchaguliwa kwa jimbo basi NEC ingetaka uchaguzi mdogo na vyama vingeshindanishwa.

Hata hivyo, katika uapisho wa leo hapakuwa na shamrashamra kama ilivyo kwa viapo vingine kwa wabunge.

Hadi sasa katika Bunge la 12, jumla ya wabunge sita wameshapoteza maisha, ikiwamo wabunge wawili wa viti maalumu ambao ni pamoja na Ndyamkama pamoja na aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Manyara, Martha Umbura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!