Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia aungana na viongozi 20 kuapishwa kwa Dk. Ruto
Habari za SiasaTangulizi

Samia aungana na viongozi 20 kuapishwa kwa Dk. Ruto

Spread the love

MACHO yote leo tarehe 13 Septemba, 2022 yanaelekezwa katika uwanja wa Kimataifa wa Moi, Kasarani Nairobi ambapo ndipo Dk. William Ruto ataapishwa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Kenya.

Dk. Ruto ataapishwa pamoja na Rigathi Gachagua, kama Rais na Naibu Rais mtawalia kwa mujibu wa sheria. Anaripoti Urumasalu Kisung’uda … (endelea).

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anaungana na baadhi ya marais wan chi mbalimbali Afrika na viongozi 20 kutoka pande tofauti za duniani, kushuhudiwa kuapishwa kwa Dk. Ruto ambaye pia alikuwa Naibu rais katika uongozi wa Uhuru Kenyatta.

Waliothibitisha kujumuika  katika hafla hiyo Rais Samia wengine ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame (Rwanda), Evariste Ndayishimiye wa Burundi, ambao ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Wengine ni Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), Salva Kiir wa Sudan Kusini, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, Nana Akufo-Addo (Ghana), Lazarus Chikwera (Malawi) na Waziri Mkuu Ethiopia, Abiy Ahmed.

Hafla hiyo pia itahudhuriwa na Ismael Guelleh wa Djibouti, Hassan Sheikh (Somalia), Azali Asoumani (Comoros), Mfalme Mswati III (Eswatini), Wavel Ramkalawan (Sychelles), Filipe Nyusi wa Msumbiji, miongoni mwa wengine.

Rais anayeondoka, Uhuru Kenyatta atamkabidhi mikoba ya uongozi Dk. Ruto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!