Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge mwingine wa upinzani akimbilia CCM
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge mwingine wa upinzani akimbilia CCM

Zubeir Kuchauka (katikati), Aliyekuwa Mbunge wa Liwale kwa tiketi ya CUF
Spread the love

ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Liwale mkoani Lindi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Zubeir amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Kuchauka ametangaza uamuzi huo leo tarehe 13 Agosti, 2018 alipokaribishwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally katika ofisi ndogo za CCM zilikoko Lumumba jijini Dar es Salaam.

“Kuanzia sasa hivi mimi sio mwanachama wa CUF kwa mtazamo huo maana yake ni kwamba , niliwahi kuwa CCM nimerejea. Narejea kwa sababu nina uhakika nimefanya utafiti wa kutosha na kubaini kuwa CCM ya Rais John Magufuli imerejea kwenye misingi ya TANU, na mimi kama mwananchi mpenda maendeleo sikuona kigugumizi kurejea,” amesema Kuchauka.

Akielezea sababu za kurejea CCM, Kuchauka amesema kupoteza mwelekeo kwa CUF kutokana na mgogoro wa kiuongozi ulioko, ndiko kulikopelekea kurudi CCM.

Tunaendelea kupokea wanachama wapya na waliorudi. Mwanachama wa upinzani akiwa mbunge zubei chauka mbunge wa cuf liwale anajiunga tena na ccm sababu aliwahi kuwa mwanaccm.

“Kwa nini nimechukua uamuzi huu leo, mnafahamu nilikuwa CUF,. Ni namna gani tumepoteza mwelekeo, mimi nimechaguliwa na wananchi, ninapokuwa huku kuna migogoro inanizuia kufanya kazi, CCM wametufanyia mambo makubwa sana. Ndio maana nimeona bora nirejee,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

error: Content is protected !!