February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli afumua wakuu wa mikoa, wakurugenzi

Spread the love

RAIS John Magufuli leo tarehe 13 Agosti, 2018 amefanya mabadiliko kadhaa kwa Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali nchini huku sehemu kubwa ya mabadiliko hayo yamelikumba Jiji la Dar es Salaam. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Uteuzi huo umetangazwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.

Mabadiliko hayo ni pamoja na uhamisho wa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Msafiri Simion aliyehamishiwa wilayani Chato, wakati Senyi Ngaga (aliyekuwa Chato) akipelekwa Kwimba.

Kwa upande wa mabadiliko ya wakurugenzi wa halmashauri, Rais Magufuli ameteua wakurugenzi 41 wapya na kuwahamisha wakurugenzi 19, akiwemo Dk. Maulid Madeni aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha huku Emanuel Mkongo akiteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Manispaa ya Meru.

Wakurugenzi waliohamishwa vituo ni pamoja na Beatrice Kwai aliyehamishiwa Manispaa ya Ubungo akitokea Manispaa ya Mtwara, wakati Jumanne Shauri alihamishiwa Manispaa ya Ilala akitokea Manispaa ya Mjii wa Korogwe.

Milabusu Ndatwa Ludigija akihamishiwa Manispaa ya Kinondoni akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.

Wakati akitangaza mabadiliko hayo, Balozi Kijazi amesema mabadiliko na uteuzi huo unaanza mara moja na kwamba wateuliwa wanatakiwa kwenda kwenye vituo vyao vya kazi mara moja.

Orodha kamili itafuata…

error: Content is protected !!