April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Chadema ahoji miradi ya maji kutokamilika

Bomba la maji

Spread the love

SERIKALI imetakiwa ieleze, ni lini itahakikisha miradi ya maji ambayo inatakiwa kutekelezwa, inatekelezwa kwa wakati. Anaripoti Dandon Kaijage, Dodoma … (endela).

Pia imetakiwa kwa namna gani miradi hiyo itaenda  sambamba na matumizi bora ya fedha, tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo hutumiwa vibaya.

Conchester Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) leo tarehe 3 Septemba 2019 amehoji serikali wakati akiuliza swali la nyongeza.

Mbunge huyo amesema, kwa kuwa serikali imetenga fedha kwa ajili ya miradi ya maji ambayo ni tatizo ya muda mrefu, je serikali inawehakikishiaje wananchi kuwa ni lini miradi hiyo itakuwa imekamilika?

Awali, katika swali la msingi la Mbunge wa Mikumu, Joseph Haule (Chadema) alitaka kujua kama serikali ipo tayari kutenga kiasi cha fedha kwenye bajeti ili kuokoa maisha ya wananchi zaidi ya 35,000.

Akijibu swali la nyongeza la Rwamlaza, Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Awesso amesema, ni kweli kulikuwa na changamoto kubwa ya kukosekana kwa maji na fedha kutotumika kama inavyotakiwa.

Hata hivyo amesema, tatizo kubwa na changamoto iliyokuwa ikijitokeza, ilikuwa ni mfumo na kwa sasa mfumo umebadilishwa na kwamba, tatizo la maji na matumizi mabaya ya fedha itabaki kuwa historia.

Akijibu Sali la msingi Awesso amesema, Kata za Ruaha, Kidodi na Ruhembe ni miongoni mwa kata 18 zilizopo katika Jimbo la Mikumi na upatikanaji huduma ya maji umefikia asilimia 68.

Aidha amesema, ni kweli chanzo cha maji cha Mto Sigaleti ni miongoni mwa vyanzo vinavyopendekezwa kutumika kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji katika jimbo la Mikumi.

error: Content is protected !!