July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai atangaza mfumo mpya kazi za Bunge 

Job Ndugai, aliyekuwa Spika wa Bunge Tanzania

Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge ametangaza kusitisha kutoa karatasi zinazoonesha orodha ya vikao vya shughuli za Bunge. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Septemba 2019 wakati akitoa tangazo kwa wabunge na kueleza, katarasi hizo hazitatumika tena ndani ya ukumbi wa Bunge na badala yake watakuwa wanatumia njia ya kimtandao.

Na kwamba, wabunge watakuwa wakipewa orodha ya shughuli za Bunge kwa kutumia njia ya mtandao.

“Nataka kuwaambia wabunge kuwa katarasi hizi ambazo tunazitumia kama kuonesha orodha ya shughuli za Bunge, leo ndio siku ya mwisho kungia humu ndani.

“Tunaanza na karatasi hizi na kwa maana nyingine tutakuwa tunawatumia kwa njia ya mtandao, sasa waheshimiwa wabunge naomba mhakikishe mnaweka namba zenu za simu vizuri, barua pepe vizuri na lengo ni kuhakikisha meza za wabunge haikai na makaratasi na badala yake zinakuwa nyeupe kabisa,” amesema Ndugai.

error: Content is protected !!