Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Mbunge atishia kukwamisha bajeti TAMISEMI kisa walemavu
Tangulizi

Mbunge atishia kukwamisha bajeti TAMISEMI kisa walemavu

Spread the love

 

MBUNGE Viti Maalumu, Stella Ikupa, ametishia kushika shilingi katika makadirio ya bajeti ya Wizara Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, endapo waziri wake, Innocent Bashungwa, hatoa maelezo ya kina juu ya halmashauri kutotoa mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ikupa ametoa msimamo huo leo Jumanne, tarehe 19 Aprili 2022, akichangia mjadala kuhusu makadirio ya bajeti hiyo, bungeni jijini Dodoma.

“Nimuombe waziri anapokuja kuhitimisha basi aweze kuelezea suala hili kwa kina, kwa nini halitekelezeki lakini pia niseme wazi maelezo ya waziri yasiponitosheleza nitashika shilingi yake, nitaondoka na huo mshahara wake,” amesema Ikupa.

Ikupa amesema halmashauri nyingi zimekuwa zikikiuka kanuni na miongozo inayoziagiza kutoa mafuta hayo kwa maalbino.

“Changamoto ya utolewaji mafuta ya watu wenye ualbino kwenye halmshauri zetu imekuwa ya muda mrefu, miongozo ipo, kanuni zinaongea wazi lakini suala hili halitekelezeki kwenye halmashari zetu, nimekuwa nikipokea simu kutoka kwa watu wenye ulemavu wakilalamikia suala hili, kwamba halmashauri hazito mafuta,” amesema Ikupa.

Ikupa amesema “Niiombe Serikali suala hili liweze kutekelezwa kwa maana ya kwamba halmashauri ziweze kutenga kununua na kusambaza mafuta haya kwa watu wenye ualbino.”

Katika hatua nyingine, Ikupa ameishauri Serikali iweke utaratibu maalumu utakaowezesha watu wenye ulemavu kupata huduma za afya bure, kama ilivyofanya kwa wazee wasiokuwa na uwezo.

“Lakini sambamba na hilo, niweke wazi watu wenye ulemavu walio wengi wanaishi kwenye kipato cha chini sana, kwa maana kwamba inapelekea kushindwa kumudu matibabu yao,” amesema Ikupa na kuongeza;

“ Niombe Serikali iweze kufanya zoezi lililofanyika kwa wazee, kuwatambua na kuwapatia vitambulisho wale ambao hawana uwezo wa kupata matibabu, ili basi vitambulisho vile viwawezeshe kutibiwa kwa urahisi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!