
Wanajeshi wa Jeshi ya DR Congo wakiwa kwenye kambi ya waasi wa ADF
Wanajeshi wawili wamewaua raia 15 kwa kuwapiga risasi katika mashambulio tofauti mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa [endelea]
Hayo yamejiri baada ya watu sita kujeruhiwa wakati wanajeshi waliporusha guruneti kwenye umati wa watu walipokuwa wakijaribu kuwakamata.
Afisa mmoja katika jimbo la Kivu Kusini, amesema mwanajeshi aliyekuwa mlevi kwenye boti la Ziwa Tanganyika amewaua abiria wanane wakiwemo Watoto kabla ya kukamatwa.
Hata hivyo siku ya jumapili tarehe 17 Aprili 2022 mwanajeshi mwingine ,alimpiga risasi kanali mmoja ,mlinzi wake na raia watano katika jimbo la Ituri .
Muuaji huyo ambaye inasemekana alikuwa mlevi alipigwa risasi na mwenzake alipokuwa akijaribu kukimbia
Kwa zaidi ya miongo miwili watu kote mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamevumilia mashambulizi ya mara kwa mara na makumi ya makundi yenye silaha.
Aidha Rais Felix Tshisekedi amesema kuwa kukomesha ghasia hizo ni kipaumbele cha kwanza kwa serikali yake
Majimbo mawili yalizingirwa kwa karibu sana mwaka mmoja uliopita
Lakini bado wanajeshi wa Congo wasio na nidhamu wanaendelea kusababisha uhalifu.
More Stories
Injinia Hersi kuanza na uwanja Yanga
Yanga hawajaacha kitu, yatwaa mataji yote msimu huu
Sopu aibuka kinara wa mabao ASFC