Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge aliyefariki alizuiwa kupanda ndege kwenda Dar
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge aliyefariki alizuiwa kupanda ndege kwenda Dar

Spread the love

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, David Kihenzile amesema siku moja kabla ya Mbunge Irene Ndyamkama kufikwa na umauti, alizuiwa kusafiri kwa ndege kuelekea mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua viwanda. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Amesema Irene ambaye alikuwa mjumbe wa kamati hiyo ya Bunge, baada ya kuzuiwa kusafiri kwa ndege alisafiri kwa gari.

Kihenzile ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 27 Aprili, 2022 wakati akitoa salamu kwa niaba ya kamati ya Viwanda ambayo marehemu Iren alikuwa mjumbe.

“Jumamosi tarehe 23, Aprili 2022 tulikuwa tunakwenda Dar es Salaam kutembelea viwanda, pamoja na hali yake aliyokuwa nayo alisema lazima ‘niende nikashiriki’. Hata hivyo tulipofika Airport Dodoma hakuweza kuendelea kutokana na logistics za hapa na pale.

“Lakini bado akasema mimi nitakwenda hata kwa gari hivyo sisi tukatangulia lakini akiwa pale alisalimia wajumbe wote wa kamati akiwa na furaha na matumaini makubwa kwamba ataungana na wenzake kukagua viwanda mbalimbali Dar es Salaam,” amesema.

Ameongeza kuwa wao (wajumbe) waliondoka Dodoma kwa ndege na walipofika Dar es Salaam, Irene alichelewa kutokana na changamoto alizozipata njia.

“Kesho yake wakati tunajiandaa kurudi tukapata taarifa kwamba mwenzetu ametanguliwa mbele za haki kwa kweli ilitusikitisha sana,” amesema.

… ALIKUWA MJAMZITO

Aidha, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Gaudensia Kabaka amesema Irene alikuwa ni mjamzito na kwamba kuna mambo mengi aliyokuwa ameyapanga kuyafanya baada ya kujifungua.

Kabaka ameeleza kuwa baada ya kutembelea ofisi za UWT aliahidi kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Katibu bwa UWT mkoa wa Rukwa baada ya kujifungua.

“Alinitembelea na kutueleza mipango yake kwa wanawake, jinsi anavyotaka kuwafanyia wanawake wa Rukwa.

“Alitueleza ameanza kujenga nyumba ya Katibu wa umoja huo mkoa wa Rukwa… na baada ya kujifungua katika uzinduzi mmoja wetu atawenda kuifanya hiyo kazi lakini imempendeza Mungu kwamba Irene hajafikia azma hiyo,” amesema.

Ndyamkama alifariki tarehe 24 Aprili, 2022 katika hospitali ya Tumbi Kibaha alikokwenda kupatiwa matibabu baada ya kuugua akiwa safari kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam na ameacha mume na watoto watatu.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!