October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kinana aitaka CCM kuwa tayari kwa maridhiano ya kisiasa

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti CCM Bara, Abdulrahman Kinana amewataka wanachama na viongozi wa CCM kuwa tayari kwa maridhiano ya kisiasa aliyoyaanzisha Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kinana ametoa kauli hiyo leo tarehe 27 Aprili, 2022 wakati akiwahutubia wanachama wa CCM kwenye ukumbi wa hotel ya Mount Meru jijini Arusha.

Kinana amesema Rais ameanzisha maridhiano kati ya CCM na vyama vyote vya siasa kwa hiyo ni lazima aungwe mkono.

“Nawaomba wana CCM wenzangu kuwa tayari kufanya maridhiano na vyama vya vya upinzani… na wao pia nawaomba wawe tayari kufanya maridhiano na CCM na kufanya maridhiano na serikali” alisema Kinana katika kauli iliyogusa mioyo ya watanzania.

Amesema Rais Samia ameonesha mfano wa mzuri na wa kuigwa kwa kuanzisha mchakato huo ambapo amekutana na vyama na taasisi mbalimbali za kisiasa.

“Juzi hapa akiwa Marekani kwenye ziara alitaja mambo manne ambayo anayashughulikia, Mariadhiano, kuvumiliana,mabadiliko kwenye taasisi na kulijenga upya taifa” alisema.

Amesema Tanzania ni nchi ya vyama vingi vya siasa kwa hiyo kuwepo kwa maridhiano ni jambo muhimu sana.

“Nchi yetu ni ya vyama vingi ni muhimu kwa vyama hivi kukaa pamoja kuzungumza.. Rais amelianza hilo na nna imani kabisa tutaelewana”

Amewataka watanzania kumuunga mkono Rais Samia katika azma yake hiyo kwani kwa kufanya hivyo Rais atafika hatua ya mbali kwenye jambo hilo.

“Bila maridhiano ni vigumu kupata maendeleo.. kwenye ugomvi hakuna maendeleo” alisema.

error: Content is protected !!