MBUNGE Viti Maalum, Janejelly Ntate, amehoji mkakati wa Serikali katika kumaliza mashtaka ya kikodi yaliyoko kwenye bodi ya rufani za kodi na baraza la rufani za kodi, ili matrilioni ya fedha zinazozibishaniwa zirudi serikalini kwa ajili ya kuhudumia wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Ntate amehoji hayo leo tarehe 10 Novemba 2023, bungeni jijini Dodoma, katika kipindi cha maswali na majibu.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, Serikali inaendelea kutekeleza mpango maalum kuanzia Novemba 2023 hadi Juni 2024, wenye lengo la kumaliza mashauri ya kikodi yaliyofunguliwa. Pia, imeunda taasisi ya msuluhishi wa malalamiko ya kikodi kwa ajili ya kupokea na kuyatatua.
Waziri huyo wa fedha amesema, amesema hadi kufikia Oktoba 2023, bodi ya rufani za kodi ilikuwa na mashauri 889 yenye kiasi cha kodi kinachobishaniwa cha Sh. 6.46 trilioni na Dola za Marekani 4.66 milioni.
Amesema bodi imeshasikiliza mashauri 167 kati ya 889 ambayo yenye thamani ya Sh. 2.66 trilioni na Dola 210,000.
Kwa upande wa Baraza la Rufani za Kodi, Dk. Mwigulu amesema kuna mashauri 176 yenye kiasi cha kodi kinachobishaniwa kiasi cha Sh. 266.94 bilioni, ambapo mashauri 91 yenye kodi Sh. 166.3 bilioni, yamesikilizwa.
Leave a comment