Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Aeshi awaonya mawaziri, ‘alilia’ meli Ziwa Tanganyika
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Aeshi awaonya mawaziri, ‘alilia’ meli Ziwa Tanganyika

Meli ya MV Liemba
Spread the love

 

MBUNGE wa Sumbawanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Aeshi Hilaly amewaomba mawaziri kutokutumia kinga ya Rais kukweka kuelezwa udhaifu wao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia, ameitaka Serikali kuwatizama wananchi wa mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa wanaotumia Ziwa Tanganyika ambao wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kutumia boti kama usafiri baada ya kutokuwapo kwa meli yoyote ndani ya ziwa hilo.

Hilaly ametoa kauli leo Jumanne tarehe 24 Mei 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Ameanza kuchangia akisema, “naomba kuwaasa mawaziri, wanaposhauriwa au tunapokosoa udhaifu wao, wasipende kuunganisha hoja zetu na kusema tunampinga Rais au tunakipinga chama au tunaipinga Serikali, wajibu wetu wabunge ni pamoja na kuishauri serikali, isije kujengenga kwamba tunaipinga serikali yetu.”

Mbunge huyo amegusia adha ya usafiri katika Ziwa Tanganyika akisema, “tumekuwa tunalia sana kuhusu usafiri wa maji ndani ya Ziwa Tanganyika na huu ni mwaka wa tatu au wa nne hakuna usafiri wa meli ndani ya ziwa Tanganyika.”

“Wananchi wanatumia maboti na wananchi wanakufa siku hadi siku, lakini kila tukija hapa unasema fedha tumetenga hela ya kujenga meli sasa tunasema hiyo meli mpya hatuihitaji sasa hivi turekebishe zilizopo,” amesema.

Aeshi amesema, “lakini jana nimeona wanakarabati meli ya MV Sangara ya kubeba mafuta badala ya kukarabati ya kubeba abiria watu wanakufa hakuna anayewajali, hakuna meli hata moja inayotembelea sasa hivi ndani ya Ziwa Tanganyika, Meli ya MV Liemba ambayo ni meli ya kihistoria imekufa haifanyi kazi.”

“Mimi nafikiri Mkoa wa Rukwa, Katavi na Kigoma tuna bahati mbaya, kila jambo tunalolipigia kelele hapa tunaambiwa litafanyika litafanyika na mwisho wa siku tukija tukipata kupinga tunaambiwa tunapingana na Serikali yetu,” amesema

“Waziri imekuwa ukituahidi sana sasa ifike mwisho wa siku uje utuambie meli itajengwa au haitajengwa, itakarabatiwa ama haitakarabatiwa ili sisi wananchi tujichange tununue meli yetu au tutumie hata ungo kusafirisha abiria wetu wanaokufa siku hadi siku,” amesema

Kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege wa Sumbawanga Mjini, Aeshi amesema ni zaidi ya miaka mitano inawekwa kwenye bajeti lakini hakuna kinachofanyika na kumwomba Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa kueleza nini kitaendelea.

“Waziri wa ujenzi alipoteuliwa mara ya kwanza kabisa aliahidi kujenga uwanja wa ndege wa Sumbawanga Mjini, ilipita kwenye bajeti hapa na sisi tukapitisha na wananchi wa Sumbawanga walifurahi sana kwamba uwanja unajengwa.”

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa

“Akatoka Mbarawa akaja waziri mwingine tukapitisha bajeti hiyohiyo ya kujenga uwanja na Sumbawanga, akatoka akaja waziri mwingine akarudi tena Mbarawa waziri wanne huyo hatujajenga uwanja na bajeti tunapitisha,” amesema na kuongeza:

“Niulize hoja kwamba tuko hapa bungeni tunapitisha bajeti ikafanyiwe kazi au tunapitisha kupoteza muda au tunataniana? Mwaka wa tano hata nusu kilomita haujawahi kujengwa na kama haupo kwenye bajeti tuelezwe kwani mwisho wa siku wananchi wanatuona hatufai na tueleze lini uwanja wa ndege utaanza kujengwa.”

Mbunge ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu amemalizia mchango wake akisema, “kuna vijimeseji meseji zinapita pita huko kuhusu ujenzi wa reli.”

“Nikanushe maana wabunge wengi wanasema ni Aeshi anaandika, mimi sijui ni Kigogo wala simjui na sijawahi kukutana naye, taarifa hii inamhusisha waziri wa fedha, nataka nitofautishe jambo hili liko wizara ya uchukuzi haliko wizara ya fedha.”

“Hoja yangu ni ya msingi tu mimi sipingani na ‘single source’ mliyotaka kufanya, napingana na utaratibu uliotumika. Hili Bunge linapaswa kuelewa mwisho wa siku tukisema jambo kuna watu wanafikiria kuna jambo limepita, kuna rushwa imetolewa mimi ni mjumbe wa kamati ya miundombinu.”

“Ninajua kila kitu kinachoendelea, mkandarasi mliyompa kutoka Isaka kwenda Mwanza hajafanya vizuri mpaka leo amejenga kwa asilimia nne lakini kwenye taarifa amesema amejenga kwa asilimia nane siyo kweli,” amesema.

Amesema “sasa hoja yangu mmempa kazi nyingine kwa single source wakati kazi ya kwanza hajafanya vizuri? Ukija waziri utupe maelezo kwa nini.”

Wakati akiendelea kuchangia, amesimama Mbunge wa Kyerwa, Innocent Bilakwate kumpa taarifa Aeshi akisema, “sisi wajumbe wa kamati ya miundombinu tumetembelea miradi na tumejiridhisha na kazi inayoendelea.”

“Na kweli kumekuwapo na kampeni na mhusika (Aeshi) amekuwa anapinga kuhusu ile kampuni na sisi kama kamati tumewaita wahusika na kutupa maelezo lakini mpaka sasa hakuna mkandarasi aliyopewa,” amesema

Alipomaliza Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu amemuuliza Aeshi kama anapokea taarifa hiyo na Aeshi akajibu, “ndio wale wale. Kama uko tayari uniruhusu nilete ushahidi na hao wajumbe waje na ushahidi wao na kama nitakuwa nimesema uongo, hatua za bunge zichukuliwe.”

“Ninachojua mimi mkandarasi amepatika kwa single source na sasa wako kwenye evaluation,” amesema.

1 Comment

  • Kweli Aeshi.
    Wanaosema unampinga raisi au Chama, wamefilisika kisiasa. Hawana hoja hivyo ni ujinga kutokujibu hoja iliyotolewa na badala yake wanaisukuma kwa raisi au chama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!