MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia, Freeman Mbowe amesema huwezi kuliacha jina la Ally Hassan Mwinyi unapotaja mageuzi nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Mbowe amesema wakati Mzee Mwinyi anaingia madarakani kama Rais wa awamu ya Pili mwaka 1985, alipokea nchi ambayo ilikua na changamoto lukuki.
“Tanzania kwa kipindi kile ilikua katika harakati za kutafuta namna bora zaidi ya kusonga mbele baada ya kipindi cha ujamaa.
“Miaka ya urais wake iliyompa jina la utani la Mzee Rukhsa ilikua msingi wa ujenzi wa taifa lenye dira na muelekeo mpya. Rais Mwinyi atakumbukwa sio tu kwa vyeo na uraisi bali pia uwajibikaji, na ubinadamu wake.
“Taifa limepoteza kisima cha busara na nembo muhimu. Natoa pole zangu dhati kwa familia, ndugu, jamaa na taifa kwa msiba huu mzito. Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un,” ameandika Mbowe.
Leave a comment