Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: CCM hawajiamini, akumbushia mil 50 kila kijiji
Habari za Siasa

Mbowe: CCM hawajiamini, akumbushia mil 50 kila kijiji

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakijiamini na kimejaa hofu dhidi ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 2 Septemba 2020, wakati akimnadi Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho pamoja na Salum Mwalimu, mgombea mwenza, kwenye uzinduzi kampeni za chama hicho Kanda ya Serengeti, mkoani Shinyanga.

Mbowe amesema, licha ya Chadema kufungwa mdomo kwa muda wa miaka mitano, bado CCM haijiamini katika uchaguzi uliokuwa huru na haki.

“Hawa wenzetu baada ya kutufunga midomo kwa miaka mitano bado wanatuogopa, hawajiamini kwenda katika uchaguzi uliokuwa huru na haki,” amesema Mbowe.

Mbowe amewataka Watanzania kufanya uamuzi sahihi katika siku ya kupiga kura, akiwataka kutorudia makosa waliyoyafanya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

“Hiki kipindi cha siku 55 kwenda uchaguzi sio cha kufanya masihara, cha kutafakari sana maumivu tuliyopitia kwa miaka mitano, tukachukue uamuzi sahihi, wala si kipindi cha kuletewa wanamuziki wanakata viuno wakati maisha yetu yanazidi kwneda kaburini,” amesema Mbowe

Mbowe amewataka Watanzania kuchagua viongozi bora ambao watakuwa waaminifu katika utekelezaji wa ahadi zao.

“Tunapoanza safari hii ya kwenda kwenye uchaguzi, tunakwenda kuchagua maisha yetu, hatuendi kuchagua bendera ya vyama, kila mmoja atafakari miaka mitano ya Kikwete (Rais Jakaya Kikwete 2005-2010) na ya Rais Magufuli, ni kipindi gani wananchi wa Shinyanga mlikuwa na maisha magumu?” amehoji Mbowe na kujibiwa ‘kipindi hiki.’

“Lakini lazima tujifunze kwa makosa tuliyofanya siku za awali, mwaka 2015 rais huyu na chama chake waliwatangazia Watanzania wote, vijiji vyote mkiwachagua kila kijiji kitapewa mil 50, zilikuja ngapi?” amewahoji wananchi waliofika katika mkutano huo ambao walijibu hakuna.

2 Comments

  • Kutoka Nairobi Kenya nawashukuru sana Mwanahamisi kutupa habari kemkem hasa za chadema maana vyombo vingi vya habari hawataki kuandika habari za Chadema sbb ya Lissuphobia,nawapenda sn jamani Mungu awalindie,#Ni yeye tuuu sio maboya wengine

  • Kutoka Nairobi Kenya nawashukuru sana Mwanahamisi kutupa habari kemkem hasa za chadema maana vyombo vingi vya habari hawataki kuandika habari za Chadema sbb ya Lissuphobia,nawapenda sn jamani Mungu awalindie,#Ni yeye tuuu sio maboya wengine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!