Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Alicia Lissu: Sitakwenda Ikulu kupika uji
Habari za Siasa

Alicia Lissu: Sitakwenda Ikulu kupika uji

Spread the love

ALICIA Magabe, mke wa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema, atakapokwenda Ikulu hatobaki kuangalia tamthilia au kupika uji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (endelea)

Alicia amewaomba Watanzania kumchagua Lissu kuwa Rais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Akihutubia mamia ya wananchi wa Shinyanga kwenye mkutano wa kampeni za urais akimwombea kura mme wake, Alicia amesema “mimi ni mtoto wa kanda hii, mimi ni mtoto wa Tarime, naomba nisema tarehe 28 Oktoba mwaka huu, pale mtakapompeleka mme wangu Tundu Ikulu, mimi sitaenda kupika uji Ikulu.

Amesema, hatokwenda Ikulu kupika uji “kwa sababu wazee wa kanda hii, waliamua niende shule nikasome na kwa taaluma yangu ya sheria kama ilivyo ya mme wangu, nitahakikisha nimepigania haki hasa za kina mama na watoto. Sitakubali kukaa Ikulu kupiga uji na kuangalia tamthilia.”

Huku akishangiliwa na mamia uwanjani hapo, Alicia amesema “mimi manyanyaso ya serikali hii nayajua, kama ni mahabusu nimekwenda, kama ni Segerea nimekwenda, nimelazimishwa kuishi nchi za watu. Kwa hiyo , mateso ya wengi nayajua si kwa taaluma bali kuyaishi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!