Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe aelezea Ndesambulo alivyofariki
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe aelezea Ndesambulo alivyofariki

Philemon Ndesamburo enzi za uhai wake akiwa na Freeman Mbowe
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupokea kwa mshutuko mkubwa wa kifo cha Muasisi wa chama hicho na mbunge wa mstaafu wa jimbo la Moshi Philimoni Ndesamburo (84), anaandika Dany Tibason.

Ndesamburo alikuwa mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini kwa mfululizo wa miaka 15 na aliamua kustaafu kwa heshima huku akiendelea kuimalisha chama pamoja akiwa na nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kanda katika mkoa wa Kilimanjaro.

Mauti yamemkuta muasisi wa chama hicho akiwa katika maandalizi ya kuandika cheki ya kiasi cha Sh. 3.5 milioni kama sehemu ya rambirambi kwa ajili ya wanafunzi 35 waliopata ajali na kupoteza maisha katika shule ya msingi ya Lackley Vicent.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Bunge, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, amesema kifo cha muasisi huyo ni msiba mkubwa kwa wanachadema na wakazi wa Mji wa Moshi kwa ujumla kutokana na jinsi alivyoweza kujenga ushirikino na umoja wakati wa utawala uongozi wake.

Akielezea juu ya kifo chake Mbowe amesema muasisi huyo alikuwa katika vikao wa Baraza Kuu la Chadema vilivyofanyikia mjini Dodoma aliweza kurejea moshi akiwa na nguvu zake bila kuwa na viashiria vyovyote vya ugonjwa.

Mbowe amesema muasisi huyo baada ya kumaliza vikao vya Baraza Kuu la Chadema, alirudi moshi na jana (juzi) alimpigia simu meya wa Jiji la Arusha Kalist Lazaro ili afike nyumbani kwake Moshi kwa ajili ya kumpatia rambirambi kwa ajili ya watoto waopata ajali na kupoteza maisha katika shule ya msingi Luckly Vicent.

Amesema Ndesamburo alimpigia meya huyo akitaka wakutane saa asubuhi jana leo (jana) na Meya alifika nyumbani kwa Ndesamburo saa nne kamili ambapo walianza kufanya mazungumzo ya kawaida pamoja na mazungumzo kwa ajili ya chama.

Aidha Mbowe amesema wakati wa maongezi hayo alitaka kujua waathirika wa ajali hiyo walikuwa wangapi na ndipo Meya alipomweleza kuwa walikuwa 35 ambapo alikuwa amekubali kutoa kiasi cha sh. laki moja kwa kila mwathirika kiasi cha jumla ya Sh. 3.5 milioni.

“Wakati Ndesamburo akianza kuandika kitabu cha cheki kwa lengo la kumkabidhi Meya kama mchango wa rambirambi kalamu ilimdondoka na kumfanya meya kumsaidia kwa lengo la kumuokotea kalamu hiyo lakini bado nguvu ziliendelea kumwishia jambo ambalo lilipelekea Meya pamoja na familia kuanza kumsaidia na kumkimbiza katika hospitali ya KCMC.

“Hata hivyo madaktari walimpokea na kuanza kumpatia msaada wa kumpatia huduma ya kumsaidia kupumua kwa mashine na majira ya saa 4:45 Ndesamburo alikata roho na kupoteza maisha, hivyo taarifa za msiba tumezipokea kwa masikitiko makubwa na ifahamike kuwa Lucy Owenya ambaye ni mbunge wa Viti Maalum ni mtoto wake alikuwa bungeni akichangia.

“Baada ya kupokea taarifa hizo tumefanya kazi ya kumtoa bungeni kwanza na kumpeleka nyumbani kwake area ‘D’ kwa ajili ya kushughulika na taratibu nyingine kwa kuzingatia kuwa mwasisi huyo pamoja na umuhimu ndani ya chama taratibu za kumsindikiza mzee wetu tunazifanya na taratibu zote zinafanyika,” ameeleza Mbowe.

Kabla taarifa ya  msiba Lucy Owenya (Chadema) akichangia ameitaka serikali ieleze ni wapi zilipo fedha ambazo serikali ilizizuia kwa maana ya DESI.

Owenya amesema serikali imseshindwa kutoa majibu ambayo yanaonesha ni wapi fedha za DESI zimepelekwa na kuhoji kuwa au pesa hizo zimeenda kufanya shughuli za serikali kama ilivyo kwa fedha za rambirambi za Arusha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!