Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha
Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the love

MASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni ya fedha katika mwaka wa fedha ulioisha wa 2022/23. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamebanika leo tarehe 28 Machi 2024, wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, anamkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan, ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha uliopita, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa CAG Kichere, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), imepata hasara ya Sh. 56.64 bilioni sawa na ongezeko la asilimia 61 kutoka hasara ya Sh. 35.24 bilioni (2021/22), licha ya kupewa ruzuku na Serikali ya Sh. 31.55 bilioni.

CAG Kichere amesema Shirika la Reli Tanzania (TRC), limepata hasara ya Sh. 100.7 bilioni, ikiwa ni pungufu ya asilimia 47.31, ikilinganishwa na hasara ya Sh. 190 bilioni, iliyopatikana 2021/22. Hasara hiyo imetokea licha ya kupewa ruzuku na Serikali ya Sh, 32.81 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Shirika lingine la umma lililopata hasara ya mabilioni ni Kampuni Tanzu ya Mafuta Tanzania (TANOIL), ambayo kwa mwaka wa fedha wa 2022/23 ilipata hasara ya Sh. 76.56 bilioni, ikiwa ni ongezeko la Sh. 68.72 bilioni kutoka hasara ya Sh. 7.84 bilioni iliyoripotiwa mwaka wa fedha uliopita.

“Hasara hii ilisababishwa na mafuta yaliyoagizwa kutoka nje kuzuiwa kwa sababu TANOIL kushindwa kulipa wauzaji na gharama kubwa ya kuhifadhia mafuta pamoja na mapato ya kampuni kupungua kwa Sh. 296,” amesema CAG Kichere.

Shirika la Posta Tanzania, nalo limeripotiwa kupata hasara ya Sh. 1.34 bilioni, ikilinganishwa na faida ya Sh. 16.21 bilioni iliyopatikana 2021/22 kutokana na shirika hilo kuuza mali zake “hasara hii imeababishwa na kupungua kwa huduma za EMS na gharama za uendeshaji kubaki kama zilivyo mwaka jana.”

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), limepata hasara ya Sh. 894 milioni, ikiwa na pungufu kwa asilimia 94, ukilinganisha na hasara iliyopata 2021/22 ya Sh. 19.23 bilioni. Hasara hiyo imepatikana licha ya Serikali kuipa ruzuku ya Sh. 4.55 bilioni na kwamba kiasi cha Sh. 4.4 ilionesha kama mapato yake kwa mwaka wa fedha ulioisha.

“Napendekeza kuwa, mamlaka za umma zinapaswa kuchukua hatua kuboresha ufanisi wa uendeshaji , kuongeza ukusanyaji mapato, kupunguza gharama na kuendeleza mkakati wa kugeuza muelekeo wa uwekezaji usiokua na ufanisi na kuhakikisha mashirika yanaendeshwa na wafanyakazi wenye weledi , ubunifu na uadilifu unaohitajika,” amesema CAG Kichere.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!