Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mangula ang’atuka CCM, Kinana arejea
Habari za SiasaTangulizi

Mangula ang’atuka CCM, Kinana arejea

Spread the love

HATIMAYE Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula ameng’atuka kwenye nafasi hiyo aliyoihudumu kwa miaka muda wa miaka 10. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Aidha, baada ya kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu wadhifa huo mbele ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa, wajumbe wa Halmashauri hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti na Rais Samia Suluhu Hassan imemteua Abdulrahman Kinana kugombea nafasi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 31 Machi, 2022, Katibu wa NEC itikadi na uenezi – CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema Mangula amewasilisha barua hiyo ya kung’atuka leo katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa CCM.

 

Amesema katika barua hiyo Mangula alimuandikia Mwenyekiti Rais Samia ambaye naye ameiwasilisha mbele ya kikao cha Halmashauri Kuu Taifa, kwa ajili ya kukidhi matakwa ya kikanuni na kikatiba.

Shaka amesema Mangula amefikia uamuzi huo ili kukidhi matakwa ya katiba ya CCM ibara ya 19 kifungu kidogo (e) ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2020 pamoja na kanuni ya 116 (d) ya kanuni ya uchaguzi wa CCM toleo la mwaka 2017.

“Kwa vifungu hivyo, baada ya kupokewa barua hiyo na kuridhiwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara imetangazwa kuwa wazi.

“Katika kukidhi matakwa ya kanuni ibara ya 105, 106 za kanuni ya uchaguzi toleo la mwaka 2017 lakini ibara 100 (5)(a) na ibara ya 114 (1) cha katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2020, makamu Mwneyekiti wa CCM atachaguliwa na mkutano mkuu wa Taifa utakaofanyika kesho,” amesema.

Amesema katika kukidhi matakwa hayo ya kikatiba, wajumbe wa halmashauri kuu Taifa baada ya kupokea ombi hilo la kung’atuka kwa Mangula katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa, wamefanya uteuzi wa mwanachama wa CCM ambaye atapelekwa kwenye mkutano mkuu kwa ajili ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.

Amesema hayo yamefanyika ili kukidhi matakwa ya Katiba ibara ya 102 (12) (a) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2020 pamoja na kanuni 106 ya uchaguzi toleo la mwaka 2017.

“Kwa hiyo kwa mnasaba huo na kwa kukidhi matakwa ya vifungu hivi, Halmashauri Kuu ya Taifa ndio yenye jukumu la kufanya uteuzi wa mwisho wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.

“Halmashauri Kuu ya Taifa imefanya uteuzi wa Abdulrahman Kinana kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Tanzania bara na uchaguzi wake utafanyika kesho kupitia mkutano mkuu maalumu wa CCM,” amesema.

Aidha, amesema Mwenyekiti wa CCM na Rais Samia amemshukuru Mangula kwa utumishi wake uliotukuka ndani ya CCM.

“Amefanya kazi ya kuwa Makamu Mwenyekiti tangu mwaka 2012 hadi 2022 ambapo kwa hiari yake leo ameamua kung’atuka ili kupisha au kutoa nafasi kwa mwanachama mwingine wa CCM ambaye atapokea kijiti hicho na kukikimbiza kwa ajili ya kuimarisha na kusogeza mbele CCM,” amesema.

Aidha, amesema wakati Mangula anang’atuka leo pia ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 81 ya kuzaliwa.

“Wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa wamemtakia kheri na baraka lakini wamemtakia maisha marefu na wamemkabidhi keki maalumu ya shukrani katika kipindi hiki cha miaka 81 ya kuwepo duniani na katika sehemu ya maisha alivyotumia kukijenga na kukipigania CCM,” amesema.

KINANA NI NANI?

Abdulrahman Omari Kinana ni mwanasiasa Mtanzania aliyewahi kuhudumu katika Bunge la Afrika Mashariki kama spika wa Bunge hilo kutoka mwaka 2001 hadi 2006.

Alikuwa katibu mkuu wa CCM kutoka mwaka 2012 mpaka hapo alipojiuzulu mwaka 2018.

Kinana aliwahi kutumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa muda wa miaka 20 akiwa na cheo cha Kanali mnamo mwaka 1972.

Alishawahi kuwa Naibu waziri wa Wizara ya ulinzi, Naibu waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.

Alishawahi kuwa Mbunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM jimbo la Arusha kwa muda wa miaka 10.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!