October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Tunisia avunja Bunge

Spread the love

RAIS wa Tunisia, Kais Saied amevunja Bunge alilokuwa amelisimamisha miezi nane iliyopita kutokana na maandamano makubwa nchini humo. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada mitandao… (endelea).

Hayo yamejiri wakati wabunge hao   wakikutana mtandaoni siku ya jumatano tarehe 30 Machi 2021 na kupiga kura ya kufuta amri za Rais ambazo zilimpa mamlaka kamili tangu mwaka 2021.

Hata hivyo, uamuzi umekuja baada ya Rais huyo kudai Bunge lilikuwa linaendeshwa kwa minajili ya kufanya jaribio la mapinduzi.

Ameseme Bunge lilipoteza uhalali wake na limesaliti Taifa hilo huku akisisitiza wabunge waliohusika watachukuliwa hatua.

Aidha, Rais Saied ameonya dhidi ya jaribio lolote la kuchochea machafuko na mgawanyo wa ndani.

Tarehe 25 Julai mwaka jana rais Saied alimfuta kazi aliyekuwa waziri mkuu Hichem Mechich na kusitisha shughuli zote za bunge.

error: Content is protected !!