Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mambosasa awaomba madereva kuwa mabalozi wa kupunguza ajali
Habari Mchanganyiko

Mambosasa awaomba madereva kuwa mabalozi wa kupunguza ajali

Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam DPA kamishna msaidizi mwandmizi wa Polisi SACP Dk. Lazaro Mambosasa
Spread the love

 

MADEREVA waliohitimu mafunzo ya udereva wa magari makubwa katika shule ya udereva kilwa road VTC Academy driving School iliyopo katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam DPA wameaswa kuwa mabalozi kwa madereva na watumaiji wengine wa Barabara ili kupunguza ajali zinazosababishwa na baadhi ya madereva wazembe hapa nchini. Anaripoti Abel Paul, Jeshi la Polisi Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 8 Novemba, 2023 na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam DPA kamishna msaidizi mwandmizi wa Polisi SACP Dk. Lazaro Mambosasa wakati akitoa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya udereva wa magari makubwa yaliyofanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja chuoni hapo.

Dk. ameongeza kuwa chuo hicho ni miongoni mwa vyuo vikongwe hapa nchini ambapo amewaomba maderva hao waonyeshe utofauti wa umahiri wao na maderva wanaosoma vyuo vingine huku akibainisha kuwa tayari serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imeendelea kuboresha bandari hapa nchini ambapo amewambia wategemee kuwepo kwa magari makubwa ambayo wataendeshwa na maderva hao walio nasifa na vigezo.

Kwa upande wake afisa mnadhimu namba moja wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam DPA Kamshna msaidizi wa Polisi, ACP Obadia Nselu amesema dereva mzuri na mahiri ni yule anayefuata sheria za usalama barabarani huku akiwaomba madereva hao waliohitimu mafunzo ya udereva katika shule ya Kilwa road VTC Academy driving School kuwa mfano mzuri wa kuigwa hapa nchini.

Naye Mratibu wa mafunzo ya udereva katika shule ya Udereva kilwa Road VTC Academy driving School mrakibu msadizi wa Polisi, ASP Martine Nyangindu amebainisha kuwa wanafunzi hao wamefundishwa mbinu mbalimbali za kuepuka ajali ikiwemo udereva kujihami ili kujilinda na kuwalinda watumiaji wengine wa Barabara.

Upendo Nnko muhitimu wa mafunzo ya uderva wa magari makubwa ameushukuru uongozi wa shule ya udereva kwa namna ambavyo wamefundishwa na kuwajengea uwezo mkubwa katika udereva wa magari makubwa huku akibainisha kuwa watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa madereva wasiofuata sheria za usalama Barabarani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!