Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Mambo magumu TRA: Maofisa waanza kudakwa
Tangulizi

Mambo magumu TRA: Maofisa waanza kudakwa

Spread the love

MAOFISA watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wanaotajwa kuhusika kuomba rushwa kwa mfanyabiashara Ramadhan Ntunzwe, watapandishwa kizimbani muda wowote kuanzia sasa. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) aliyoitoa tarehe 10 Juni 2019, imeanza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli.

Mnamo tarehe 7 Juni 2019 alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara Ikulu, jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli aliagiza TAKUKURU kufuatilia sakata la Ntunzwe.

Ni baada ya mfanyabishara huyo wa Kariakoo mbele ya Rais Magufuli kudai kwamba, mizigo yake ilizuiwa tangu mwaka 2016 huku akidaiwa kutoa rushwa. Pia amelalamikia ukadiriaji wa kodi kwa bidhaa za mmiliki wa kampuni ya Steps Entertainment.

CP. Diwani Athumani, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kupitia taarifa hiyo amesema, taasisi yake itawafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu watumishi watatu waliohusika na ukamataji pamoja na uzuiaji wa mzigo wa Ntunzwe kwa makosa ya rushwa.

Taarifa hiyo ya CP Athumani imewataja watuhumiwa hao kuwa ni, Charity Ngalawa Mtumishi wa TRA makao makuu, Simon Sungu pamoja na Ramadhan Uweza ambao wote ni Askari Polisi wa Kituo cha Polisi Oysterbay mkoa wa Kinodnoni jijini Dar es Salaam.

“Watuhumiwa hawa kw apamoja watafikishwa mahakamani leo kujibu shtaka la kuomba rushwa ya Sh. 2 milioni kutoka kwa Ntunzwe kinyume cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007,” inaeleza sehemu ya taarifa ya CP Athumani.

CP Athumani amesema TAKUKURU imechukua hatua hiyo baada ya uchunguzi wake kubaini kwamba watuhumiwa hao waliomba rushwa ili waweze kuachia mzigop wa mfanyabiashara huyo, walioukamata kwa madai ya kufanya udanganyifu wa kiwnago cha bidhaa alizonazo na kukithiri ukadiriaji wa kodi.

Kuhusu sakata la Step Entertainment, CP Athumani amesema TAKUKURU inawashikilia watumishi wanne wa TRA mkoa wa Ilala wanaohusika na ukaguzi na ukadiriaji wa kodi kwa ajili ya uchunguzi dhidi ya ukaguzi na ukadiriaji walioufanya kwa bidhaa za Mfanyabiashara Dilesh Solanki ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo ya sanaa.

CP. Athuman amesema watumishi hao wanachunguzwa kwa kosa la kutumia madaraka yao vibaya kinyume cha sheria, ambapo wanadaiwa kutoa makadirio ya juu ya kiasi cha Sh. 3.1 Bilioni  kama kodi za bidhaa mbalimbali za mfanyabiashara huyo.

Kwa upande wa tuhuma za unyanyasaji na madai ya rushwa kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Tumbaku Morogoro, CP Athuman amesema TAKUKURU imeiongeza nguvu ya timu ya uchunguzi wa tukio hilo ambayo imeshaanza kazi mkoani Morogoro.

“Uchunguzi dhidi ya tuhuma hii utakapokamilika tutatoa taarifa,” amesema CP. Athuman.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!