Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai awananga wapinzani
Habari za Siasa

Spika Ndugai awananga wapinzani

Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge ametumia ujio wa Mukabalisa Donatile, Spika wa Bunge la Rwanda kuwanaga wapinzani nchini. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Spika Ndugai akizungumza bungeni jijini Dodoma wakati wa kumtambulisha Spika Donatile leo tarehe 10 Juni 2019 amesema, wapinzani wa Rwanda hapingi kila kitu kama walivyo wapinzani wa Tanzania.

Spika Ndugai amesema, Rwanda iko tofauti na Tanzania kutokana na kuwa na vyama vya ushindani na si vya kupinga kila kitu.

“Tofauti na hapa kwetu ni kwamba, Spika wa Rwanda kwenye Katiba yao anatoka chama tofauti na tawala, lakini niseme kwamba Rwanda hawana vyama pinzani vya kupinga kila kitu kama hapa.

“Wao wana vyama ushindani tofauti kubwa ni hapo, kile cha kupinga na kubisha haiwezekani,” amesema Spika Ndugai.

Spika Donatile aliwasilisi nchini jana tarehe 9 Juni 2019 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, ikiwemo kukutana na wabunge, kamati mbalimbali za Bunge, Chama cha Wabunge Wanawake (TGWP).

Pia, atafanya ziara katika maeneo mbalimbali jijini Dodoma na kumtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!