Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Makonda amrithi Mjema uenezi CCM
Habari za SiasaTangulizi

Makonda amrithi Mjema uenezi CCM

Paul Makonda
Spread the love

HATIMAYE aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akichukua nafasi ya Sophia Mjema. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Pia halmashauri hiyo iliyokutana leo tarehe 22 Oktoba, 2023 mjini Dodoma, katika ikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan, imeridhia kuielekeza Serikali kuendelea na hatua ya utiaji saini mikataba ya uendelezaji na uwekezaji wa bandari.

Katika taarifa iliyotolewa na Idara ya Itikadi na Uenezi CCM, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kwa kumteua Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi.

Makonda amechukua nafasi ya Sophia Edward Mjema ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake, Watoto na Makundi Maalum.

Pia Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pia imemteua Rabia Abdallah Hamid kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI).

Rabia amechukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!