Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Makonda ampa miezi sita Majaliwa, awarushia dongo kina Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

Makonda ampa miezi sita Majaliwa, awarushia dongo kina Mbowe

Spread the love

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amempa miezi sita Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, atatue migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Makonda ametoa agizo hilo leo tarehe 1 Novemba 2023, akizungumza na wananchi wa Jiji la Dodoma.

Mbali na agizo hilo kwa Waziri Majaliwa, Makonda amempaka miezi miwili Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa, kuhakikisha anatafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo.

“Chama kinamuelekeza waziri mkuu kusimamia kikamilifu suala la kutatua migogoro kwa kuunganisha wizara tatu, ardhi, maliasili na TAMISEMI. Chama kinamtaka waziri Majaliwa ndani ya miezi sita awe amesimamia na kuratibu kikamilifu kuondoa na kufuta migogoro ya ardhi,” amesema Makonda.

Katika hatua nyingine, Makonda amemtaka Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo jijini Dodoma, akisema asilimia 49 ya wananchi wake hawapati maji safi na salama.

Katika hatua nyingine, Makonda amewataka wapinzani huku akiwataja, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na makamu wake, Tundu Lissu, kama wana kero zao waziwasilishe CCM ili zifanyiwe kazi.

“Vyama vya watoa taarifa wasisite wanapokuwa na jambo lolote lile ambalo wanaliona chama tawala linaweza kulifanyia kazi, sababu sote tunajenga nyumba moja na Rais wetu anataka nchi kue. Watoa taarifa mnavyokuwa na taarifa mahususi kaka angu Lissu, Lema na Mbowe, hata kama mimi mnaogopa kunipa taarifa kuna wazee wafikishieni na tutaliangalia,” amesema Makonda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!