Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makonda adai kuna watu wanapanga kumuua kwa sumu
Habari za Siasa

Makonda adai kuna watu wanapanga kumuua kwa sumu

Spread the love

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amedai kuna watu wanapanga njama za kumuuwa kwa sumu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Songwe…(endelea).

Akizungumza katika ziara yake Tunduma, mkoani Songwe, Makonda amedai uamuzi wake wa kusema kweli bila kumung’unya maneno umewafanya baadhi ya watu kumtegemea sumu ili wamuondoe.

“Si nimepewa usemaji? nitasema kweli bila kumung’unya maneno na kwa taarifa yenu sifi na Mungu hana mpango wa kuniondoa kwanza, mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu, mtafute waganga mnapoteza muda tu, nataka kila Kiongozi awajibike kwenye nafasi yake,”  amesema Makonda.

Msemaji huyo wa CCM amedai baadhi ya wanaopanga njama kumuuwa ni watendaji wa serikali.

“Waliopo Serikalini wote wana magari, nyumba na wanaheshimika kwa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kwanini hatumsaidii kazi?, tabia ya kusubiri Rais ana ziara ndiyo mnajitokeza na mkifika pale ooh Mama unaupiga mwingi hapa ni wewe tu!, ngojeni dawa yenu inachemka,” amesema Makonda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!