Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia apangua, ateua wakurugenzi taasisi za umma
Habari za Siasa

Samia apangua, ateua wakurugenzi taasisi za umma

Spread the love

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wanne katika taasisi mbalimbali ikiwa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumanne na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imesema Rais Samia amemtea Dk. Thomas Nestory Bwana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

Dk. Bill Kiwia

Kabla ya uteuzi huu Dk. Bwana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Mazingira (Biodiversity Conservation) Ofisi ya Makamu wa Rais. Anachukua nafasi ya Dk. Geofrey Mkamilo ambaye amemaliza muda wake. Ameongeza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 3 Februari 2024.

Pia amemteua Abdul-Razag Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Kabla ya uteuzi huu Badru alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB).

Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba atapangiwa kazi nyingine.

Pia Rais Samia amemteua Dk. Bill Kiwia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Dk. Kiwia anachukua nafasi ya Badru ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Uteuzi huu unaanza leo tarehe 6 Februari 2024.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!