Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makonda adai kuna mtandao wa vigogo unaodhulumu wanyonge
Habari za Siasa

Makonda adai kuna mtandao wa vigogo unaodhulumu wanyonge

Paul Makonda, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

 

KATIBU wa Itadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amedai ziara yake aliyoifanya hivi karibuni katika mikoa kadhaa, imebainisha kwamba dhulma imekithiri hasa kwa wananchi wanyonge wanaoporwa haki zao na watu wenye pesa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 5 Machi 2024, jijini Dar es Salaam, Makonda amedai kuna mtandao wa watu wenye fedha wanaowatumia baadhi ya viongozi serikjali kudhulumu haki za wanyonge hasa katika sekta ya ardhi.

“Hawa watu wanaotapeli ardhi za watu hawafanyi peke yao, wanayo mitandao mikubwa inayowalinda kwa sababu si pesa tu, lazima uwe na pesa na watu wanaopokea fedha zao katika kudhulumu haki za watu,” amesema Makonda.

Makonda amesema mbali ya dhulma katika sekta ya arhdi, ziara yake imebaini kuna dhuluma katika biashara kati ya mtu na mtu na baadhi ya watu kujipatia mali kwa njia za udanganyifu.

Amesema kumekuwa na changamoto za baadhi ya watendaji wa serikali kutotatua changamoto za wananchi, kitendo kinachopelekea CCM kupokea watu 100 hadi 200 kwa siku ambao wanafika ofisini za chama hicho kufikisha malalamiko yao.

“Tatizo tulilonalo ni kutokutatua kero za wananchi na ndio maana kila ukienda utaambiwa nilienda kwa fulani na fulani, kweli tumejikuta tuna mambo mengi hapa kwenye makao makuu Lumumba na Dodoma ofisi yetu inapokea watu wengi sana kwa siku wanafika 100 mpaka 200 na wote ukiwasilikiza wanakwambia nimeenda kwa fulani hakuna jibu nililopata,” amesema Makonda.

Makonda amesema ziara yake aliifanya kwa lengo la kutekeleza ibara ya 160 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM, inayokielekeza chama hicho kuisimamia serikali katika utekelezaji wa masuala ya utawala bora, utawala wa kisheria na upatikanaji wa haki kwa wananchi.

“Ni wajibu wetu kuhakikisha wananchi wanapata majibu ya changamoto zao kwa hiyo tuliyobaini katika ziara kwamba kwa kiwango kikubwa dhulma imekithiri, mioyo ya watanzania wengi wameumizwa na dhulma na imegawanyika kwenye maeneo mengi na ni wajibu wetu kuielekeza serikali ili ipambane na dhulma inayowatenda na kuwakandamiza wananchi hasa walio wanyonge,” amesema Makonda.

Makonda amesema CCM kinaagiza watendaji wa serikali kuwachukulia hatua wale wote wanaodhulumu haki za wanyonge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!