Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara Makamu Rais AngloGold Ashanti-GGML atembelea maonesho ya madini Geita
Biashara

Makamu Rais AngloGold Ashanti-GGML atembelea maonesho ya madini Geita

Spread the love

MAKAMU Rais wa kampuni ya AngloGold Ashanti Tanzania-GGML anayeshughulikia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo leo Ijumaa ametembelea maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita na kupata maelezo kutoka kwa washiriki mbalimbali wa maonesho hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mbali na kutembelea banda la Geita Gold Mining Limited (GGML) ambao ni wadhamini wakuu wa maonesho kwa mara nyingine mwaka huu, pia ametembelea banda la linalotoa huduma za elimu na uchunguzi wa saratani kwa wananchi wote mkoani Geita.

Makamu Rais wa kampuni ya AngloGold Ashanti Tanzania anayeshughulikia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Geita Gold Mining Limited (GGML) alipotembelea banda la kampuni hiyo leo Ijumaa.

Banda hilo linalotoa huduma bure za uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume, limeratibiwa na Kampuni ya GGML kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.

Pia Shayo amepata maelezo kutoka kwa Mratibu wa huduma za Tiba  Hospitali ya Rufaa ya mkoa Geita, Dk. Pasclates Ijumba ambaye amemueleza kuwa mbali na uchunguzi wa saratani hizo pia wananchi wataatiwa elimu ya kutosha namna ya kujikinga na maradhi hayo.

Makamu Rais wa kampuni ya AngloGold Ashanti Tanzania-GGML anayeshughulikia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo akisaini kitabu cha wageni katika banda la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) lililopo kwenye maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita.

“Tunatoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hii hasa ikizingatiwa tatizo la saratani bado linakua kila mwaka hivyo ni vema kuwahi kufanya uchunguzi na kupata matibabu mapema na kuitibu kabisa lakini ukichelewa haitibiki na matibabu yake ni gharama kubwa kwa jamii yetu,” amesema.

Makamu Rais wa kampuni ya AngloGold Ashanti Tanzania-GGML anayeshughulikia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo akipata vipimo katika banda linalotoa huduma bure za uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume. Huduma hiyo imeratibiwa na Kampuni ya GGML kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.

Katika maonesho hayo ambayo mwaka huu yamejumuisha zaidi ya washiriki 400, yatafanyika kwa muda wa siku 10 kuanzia tarehe 20 hadi 30 Septemba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cheza sloti ya Zombie Apocalypse na ushinde kirahisi

Spread the love Wengi wetu hupenda filamu za Mazombie huwa zinatishakidogo lakini...

Biashara

Ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu katika utekelezaji wa sera za afya na usalama kazini

Spread the love  KILA ifikapo Aprili 28 ya kila mwaka, dunia huadhimisha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Biashara

Wazir Jr kinara wa ufungaji KMC FC ajiunga Meridianbet

Spread the love    MUITE Wazir Jr ‘The King of CCM Kirumba’,...

error: Content is protected !!