Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makamu Othman: Hatutaki uongozi fisadi, wa uongo
Habari za SiasaTangulizi

Makamu Othman: Hatutaki uongozi fisadi, wa uongo

Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Zanzibar
Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, Othman Masoud Othman amesema uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimboni Mtambwe, unaooigwa kesho, ni alama na dira ya kule Wazanzibari wanakotaka kupelekwa. Anaripoti Jabir Idrissa, Wete, Pemba … (endelea).

Othman ambaye pia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema wananchi wa Zanzibar hawataki tenda kuendeshwa kifisadi wala kinafiki.

Amesema wanataka utamaduni mpya wa kuendeshwa uchaguzi kihaki na kwa mujibu wa ustaarabu wanaojinasibu nao kama mwenendo mwema wa kizazi na kizazi.

Akielekeza msimamo wake kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, anayetimiza miaka mitatu ya uongozi wake Zanzibar, Othman amemsihi kama kweli ni muumini wa amani ya kweli katika nchi anayoongoza serikali, basi awe mstari wa mbele kukemea ubadhirifu, ufisadi, uongo na unafiki. Na aongoze kwa kufuata misingi ya haki pasina kujali maslahi ya kisiasa.

“Tumeendekeza ufisadi katika nchi; sisi dhamira yetu ni kuimarisha utawala bora ambao msingi wake mkuu ni utekelezaji wa haki, vinginevyo ni kukumbatia ufisadi, unafiki, uongo na ubadhirifu hivyo kuibomoa nchi. Leo tunaona mpaka wakuu wa mikoa wana ufisadi mkubwa,” alisema wakati akifunga kampeni ya chama hicho uwanja wa Daya, Mtambwe, Wete, Kaskazini Pemba.

Wananchi wa jimbo la Mtambwe wanatarajiwa kupiga kura tarehe 28 Oktoba ya kumchagua Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi baada ya kufariki dunia kwa Habib Mohamed wa ACT Wazalendo, Julai mwaka huu.

Huu unakuwa ni uchaguzi mdogo wa nne tangu 2020, ukianzia na ule wa Pandani ambako aliyekuwa mwakilishi, Aboubakar Khamis Bakary, alifariki dunia kutokana na tukio la kupigwa risasi mguuni wakati wa uchaguzi mkuu.

Akikumbushia uendeshaji uchaguzi mdogo majimbo ya Konde, Pandani na Amani, Othman anasema ulikuwa ni ishara ya ukiukaji mkubwa wa misingi ya haki, badala yake dalili za maandalizi ya vurugu kama inavyoonekana hadi sasa.

Hivi karibuni akiwa kwenye ziara ya mikutano ya hadhara ya chama, Othman aliwahi kukemea mipango ya kuvuruga uchaguzi na akataka Jeshi la Polisi kuwajibika kikatiba kwa kuzuia mipango hiyo, si hivyo “vurugu itakuja kuwa kubwa na watakuja kujibu.”

Akihutubia mkutano wa ufingaji kampeni, Ismail Jussa Ladhu ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, alisema wananchi wa Zanzibar hawadanganyiki kwa sababu tayari ni weledi wa siasa, jambo alolithibitisha Jaji Joseph Warioba aliposema “Wazanzibari hasa watokao Pemba hawana ulazima wa kufundishwa siasa, wanaijua na wanao msimamo imara na uchungu khasa na nchi yao.”

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!