Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa: Serikali haitawatupa wakulima wa tumbaku
Habari za Siasa

Majaliwa: Serikali haitawatupa wakulima wa tumbaku

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita haitawatupa wakulima wa tumbaku na amewataka waongeze uzalishaji kwani soko la uhakika lipo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma …(endelea).

Ametoa kauli hiyo jana jioni tarehe 18 Oktoba, 2022 wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku wilayani Namtumbo kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya Nasuli, wilayani humo. Wadau hao wanajumuisha wakulima, wanunuzi, wenye viwanda, maafisa kilimo, wasambazaji mbolea na wenye mabenki.

Waziri Mkuu amewapa maagizo viongozi wa mkoa na wilaya wahakikishe kuwa pembejeo za kilimo zinazotolewa na Serikali kwa njia ya ruzuku zinawafikia walengwa na hakuna ubadhirifu unaofanywa.

Akitoa maelekezo kwa viongozi wa mkoa wa Ruvuma, amewataka washirikiane na Wizara ya Kilimo kusimamia upatikanaji wa huduma za ugani kwa wakati ili wakulima waweze kuzalisha kwa tija. “Maafisa Kilimo walio chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI na wale walio Wizara ya Kilimo waratibiwe na kusimamiwa kwa pamoja ili wafanye kazi ya kuwahudumia wakulima kwa ufanisi,” amesisitiza.

Pia ametaka kuwepo na mikakati madhubuti ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kufikia malengo yaliyowekwa na kusisitiza kuwa wakulima wa tumbaku waelimishwe kufuata mbinu bora za kilimo ili wazalishe kwa tija. 

“Bodi ya Tumbaku isimamie upatikanaji wa pembejeo na kuhakikisha zinawafikia wakulima kwa wakati. Kwa kuwa msimu wa uzalishaji wa tumbaku umeanza, pembejeo katika zao hilo ziharakishwe kuwafikia wakulima,” amesisitiza.

Kuhusu malipo kwa wakulima wa zao hilo, Waziri Mkuu ametaka usimamizi wa malipo ya wakulima uimarishwe ili wakulima walipwe kwa wakati. “Masoko ya uuzaji wa tumbaku yaimarishwe sambamba na kutatua changamoto zilizopo ili wakulima wa tumbaku wapate tija zaidi,” ameongeza.

Awali, Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Mazao ya Kilimo cha Songea Namtumbo (SONAMCU), Juma Mwanga alimweleza Waziri Mkuu kwamba chama chao kimeongeza hamasa kwa vyama vya msingi ili wakulima zaidi walime tumbaku na waweze kukidhi mahitaji ya soko.

“Tulikuwa na wanachama 46 lakini katika msimu wa 2022/2023 tumehamasisha vyama vya msingi 62 na vyote vimeahidi kulima zao la tumbaku.”

Pia alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruzuku ya mbolea ili kumpunguzia mzigo mkulima. “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa ruzuku ya mbolea kwani bei ya mfuko mmoja ni sh. 70,000 ukienda popote pale hapa wilayani.”

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku, Victor Mwambalaswa alisema kuwa uzalishaji wa tumbaku nchini umeongezeka kutoka kilo milioni 60 hadi kilo milioni 108. “Kimkoa, uzalishaji umeongezeka kutoka kilo 500,000 hadi milioni kilo milioni 9.2.”

Alisema ongezeko hilo la uzalishaji linahitaji kuongezwa kwa miundombinu ya mabani, vichanja na maafisa ugani wa kuwasaidia wakulima.

Wakati mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa (CCM) alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufungua mahusiano ya kibiashara na nchi za nje hali ambayo alisema imesaidia kupata wanunuzi wa zao hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!