Tuesday , 16 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanne mbaroni kwa kukutwa na simu ya ofisa wa tume uchaguzi aliyeuawa
Kimataifa

Wanne mbaroni kwa kukutwa na simu ya ofisa wa tume uchaguzi aliyeuawa

Pingu
Spread the love

WATU wanne wamekamatwa jana tarehe 18 Oktoba, 2022 baada ya kupatikana na simu ya mkononi ya Daniel Musyoka – Ofisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya aliyeuawa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Polisi walisema waliwakamata wanne hao kama washukiwa huku wakiendelea kuchunguza mauaji ya Musyoka ambaye mwili wake ulitupwa katika eneo la Loitoktok, Kajiado tarehe 15 Agosti, 2022 siku chache baada ya kutekwa nyara na watu wasiojulikana kutoka kituo cha kujumuisha kura cha Embakasi nchini humo.

Alikuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa eneo la Embakasi Mashariki katika uchaguzi wa tarehe 9 Agosti, 2022.

Polisi walisema washukiwa waliokamatwa walikutwa na simu ya marehemu ambapo pamoja na mambo mengine walifuta taarifa zake kabla ya kuiuza kwa mwanamke asiyefahamu chochote kuihusu huko Kisii.

Washukiwa hao ni pamoja na mafundi watatu wanaotengeneza simu za mkononi katika jiji la Nairobi.

Wapelelezi katika kesi hiyo walisema walimtafuta mwanamke huyo huko Kisii na kupata simu hiyo kabla ya kuwakamata wanaume wengine waliokuwa wameshughulikia kifaa hicho.

Mmoja wa washukiwa aliambia polisi kuwa aliichukua simu hiyo katika Mombasa Road tarehe 14 Agosti, 2022, ambayo ilikuwa siku tatu baada ya Musyoka kutoweka.

Kisha akaipeleka kwa mafundi wa katikati ya jiji kwa ajili ya matengenezo.

“Anasema hakujua simu hiyo ilikuwa ya mtu aliyeuawa na kwamba aliipeleka kwa watu wanaotengeneza vifaa vyake kabla ya kumuuzia mwanamke huyo,” afisa wa polisi anayefanya uchunguzi huo alisema.

Mwanamke huyo alihojiwa na kuachiliwa kwani polisi wanaweza kumtumia kama shahidi.

Aliwaambia polisi kuwa mwanafamilia alimnunulia na alikuwa ameitumia kwa mwezi mmoja.

Wapelelezi hao walisema hawaamini kuwa wamewapata wauaji wakuu wa Musyoka lakini uchunguzi unaendelea.

Wanne hao wamefikishwa katika mahakama ya Makadara leo tarehe 19 Oktoba, 2022 na polisi wameomba siku zaidi chini ya ombi tofauti la kuwazuilia huku wakiendelea na uchunguzi.

Uchunguzi wa mwili wa Musyoka ulionyesha kuwa alinyongwa. Pia alikuwa na majeraha ya mwili.

Polisi bado wanachunguza kisa hicho. Wanafamilia wa Musyoka walidai kuwa huenda aliuawa kwa kukataa kupokea hongo.

Polisi wamewataka wawe na subira huku uchunguzi ukiendelea. Walionya umma kuwa makini katika ununuzi wa bidhaa ambazo zimetumika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

Habari za SiasaKimataifa

Rais Faye amteua aliyekuwa mfungwa mwenzie kuwa waziri mkuu

Spread the loveRais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ousmane Sonko...

error: Content is protected !!