September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa: Mikoa, wilaya mpya hadi sensa ifanyike

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali imesitisha utaratibu wa kugawa mikoa, wilaya, kata, vijiji vipya hadi hapo sensa itakapofanyika mwaka 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo tarehe 9 Septemba bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Aleksia Kamguna (CCM).

Mbunge huyo alihoji ni lini mikoa ya Tabora, Tanga na Morogoro itagawanya kwa kuwa ni mikoa mikubwa hali iliyosababisha huduma za kijamii kama vile afya kudorora.

Akijibu swali hilo Majaliwa alikiri kuwa ni kweli mikoa hiyo ni mikubwa sana ikilinganishwa na mikoa mingine na taarifa kwa maandishi imekwishawasilishwa serikalini.

“Serikali tulisitisha kutoa maeneo mapya ya utawala kutaka kuimarisha maeneo mapya ambayo ni vijiji, kata, wilaya na mikoa ili kuwe na miundombinu ya kutosha na watumishi.

“Pia tumesitishaili tunasubiri sensa ya mwaka 2022 ili kupata takwimu halisi ya idadi ya wakazi itakayoturahisisha kufanya uamuzi kulingana na ukubwa wa eneo kwa kuzingatia vigezo tunavyotumia. Baada ya sensa itafanya maamuzi,” amesema.

error: Content is protected !!