Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari Majaliwa aagiza wizara kuacha ubaguzi ajira za wahitimu JKT
Habari

Majaliwa aagiza wizara kuacha ubaguzi ajira za wahitimu JKT

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuendelea kutangaza ajira katika vyombo mbalimbali vya dola kwa kufanya mchujo kwa wahitimu wote wa mafunzo kutoka Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia mwaka 2015. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo tarehe 9 Septemba jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Chadema, Esther Matiko.

Matiko alihoji kwanini wizara ya mambo ya ndani ya nchi imewaacha wahitimu wa mafunzo hayo ambao hawakuwa kuajiriwa tangu mwaka 2015/2016 badala yake imekuwa ikiajiri waliohitimu katika siku za karibuni pekee.

Matiko aliongeza kuwa hali hiyo imechangia upungufu mkubwa wa watumishi kwenye vituo vya polisi ambapo baadhi sasa vinafungwa.

Akijibu swali hilo, Majaliwa aliiagiza wizara ya mambo ya ndani ianze kuchuja wahitimu kuanzia wa mwaka 2015/2016 maarufu kama Operesheni Magufuli ili nao wapate ajira kama wana sifa zinazihitajika.

“Serikali itawaita wote iwachuje na waziri wa mambo ya ndani yupo hapa, atachukua hili kwa ajili ya kulifanyia kazi,” alisema.

1 Comment

  • Aya bwana. Hebu tuendelee kupambana na mifumo hii.

    Asante sana kwa kutuhabarisha. Ina maana tangazo la Vigezo vya ajira za polisi halikuwa wazi mpaka maelekezo yanatolewa baada ya kufungwa kwa dirisha la kutuma maombi.

    Zaidi ya yote asante sana Waziri mkuu na Mbunge Esther Matiko.

    Asante kwa kuhabarisha.

    Rafiki yako,

    Aliko Musa.

    Real estate investment consultant

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!