September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

RC Dar ashusha rungu kwa machinga

Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amepiga marufuku ufanyaji wa biashara maeneo watembea kwa miguu hifadhi ya barabara zote za mkoa huo baada ya utaratibu huo kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani na ongezeko la ajali. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

RC Makalla ametoa maaagizo hayo leo Alhamisi, tarehe 9 Septemba 2021, alipotembelea Soko la Kariakoo na kujionea kero ya Ufanyaji biashara holela Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.

Kutokana na hilo, amewaelekeza mkuu wa wilaya ya Ilala kufanya kikao na wafanyabiashara hao Jumatatu tarehe 13 Septemba 2021 na kuainisha maeneo ya kuwapeleka wote waliovamia hifadhi ya Barabara.

Aidha RC Makalla amewaelekeza kuangalia utaratibu mzuri wa kufunga na kufungua baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya biashara Kutokana na ufinyu wa maeneo ili Waweze kupata riziki.

Hata hivyo, amesema kwa tathimini aliyofanya amebaini hali ya ufanyaji biashara holela Dar es salaam ipo kwa kiwango kikubwa na kuwanyima watembea miguu haki zao za msingi.

Pamoja na hayo, RC Makalla ameelekeza manispaa zote za mkoa huo kuweka vibao vya kuzuia biashara kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.

error: Content is protected !!