WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi watumie huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid Campaign), kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Majaliwa ametoa wito huo jana Alhamisi, akizindua kampeni hiyo kwa mkoa wa Dodoma, inayoanza leo tarehe 28 Aprili 2023, katika halmashauri nane mkoani humo ikiwemo Mpwapwa, Kondoa, Bahi na Dodoma Mjini.
“Kampeni hii itasadia kuboresha upatikanaji wa haki kwa watu wasiojiweza, hususan wanawake, watoto na makundi mengine yaliyo katika mazingira magumu. Vilevile itachangia kuimarisha amani na utulivu, kuongeza kipato na kuleta utengamano wa kitaifa,” amesema Waziri Majaliwa.
Majaliwa amesema kampeni hiyo itasadia kuimarisha mfumo wa utoaji Huduma za msaada wa kisheria kuanzia Serikali kuu hadi Serikali za Mitaa.
Aidha, Majaliwa ameiagiza Wizara ya Katiba na Sheria, iweke mfumo mzuri wa kushighulikia changamoto za kisheria zitakazoibuliwa wakati wa kampeni hiyo.
Katika kampeni hiyo, kata 80 na vijiji 240, vinatarajiwa kufikiwa na kampeni hiyo, iliyozinduliwa kitaifa tarehe 15 Februari mwaka huu.
Kampeni hiyo inayotekelezaa chini ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Shirika la Legal Services Facility (LSF) na mashirika mengine, imepewa jina la Samia, ili kuenzi mchango wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika kutokomeza vitendo vya ukatili hasa kwa kina mama, watoto na makundi Maalum.
Kampeni hiyo inafanyika kwa miaka mitatu mfululizo, kuanzia Machi 2023 Hadi Desemba 2025.
Leave a comment