Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Majaliwa awa mbogo Tanzania kupigwa ‘bao’ uzalishaji Tanzanite
Habari Mchanganyiko

Majaliwa awa mbogo Tanzania kupigwa ‘bao’ uzalishaji Tanzanite

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, imeagiza Wizara ya Madini, ihakikishe taratibu za uuzaji madini ya Tanzanite, zinafanyika katika mgodi unaozalisha madini hayo, ili kudhibiti nchi zinazojitangaza kuwa wazalishaji wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Jumatano, tarehe 7 Julai 2021, akizindua Kituo cha Tanzanite cha Magufuli, kilichopo katika mgodi wa madini hayo, Mirerani mkoani Manyara.

Kituo hicho kimepewa jina la aliyekuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, aliyefariki dunia tarehe 17 Machi 2021 na kuzikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita, tarehe 26 Machi mwaka huu.

“Tanzanite inazalishwa hapa Mirerani nchini Tanzania na ni rasilimali yetu. Tumeweka sheria hakuna kutoka hapa, mteja aje hapa. Tanzanite inapatikana hapa na ni keki lakini tunapoteza legacy hii ya kumiliki. Wengine wanatangaza sisi wazalishaji,” amesema Waziri Majaliwa.

Waziri Majaliwa ameongeza “malengo yetu kuhakikisha kwamba haya madini taratibu zote ziishie hapa Mirerani, tunaweza karibisha watu wakakaa hapa. Wizara kamilisheni taratibu hizo ili nchi itambulike kimataifa.”

Waziri mkuu huyo wa Tanzania, ameagiza wizara hiyo ikamilishe haraka zoezi la utungaji kanuni za kuratibu shughuli za uchimbaji na uuzaji madini hayo, ili kudhibiti nchi zinazojitangaza kuwa wazalishaji madini hayo.

“Lengo la Serikali madini haya yatambulike yanatoka Tanzania, kuna wanaojitangaza yanatoka kwao katika soko la dunia. Wizara malizeni haraka uundwaji kanuni, zitasaidia kuondoa changamoto hii,” amesema Waziri Majaliwa.

Awali, Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila, alisema wizara hiyo imeshaandaa kanuni hizo, lakini hazijaanza kutekelezwa kwa kuwa zilikuwa na dosari.

Prof. Msanjila alisema marekebisho ya kanuni hizo, yatakamilika ndani ya wiki moja kuanzia sasa. Pia, amesema Wizara ya Madini imeunda kamati maalumu kwa ajili ya kusimamia shughuli za Tanzanite.

“Ndani ya wiki moja, hizi kanuni zitaanza kutumika na tunaweka kipaumbele kwamba biashara ya madini ifanyike eneo la Mirerani pekee,” amesema Prof. Msanjila.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 120 za DMDP zaibadilisha Ilala, wananchi watoa ya moyoni

Spread the loveJUMLA ya Sh bilioni 120.7 zimetumiwa na Halmshauri ya Jiji...

error: Content is protected !!