May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Wimbi la tatu corona lipo Tanzania, Dar na Arusha…..

Spread the love

 

SAMIA Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania amesema, wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19), limetua nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amewataka wananchi katika maeneo mbalimbali, kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya corona ikiwemo kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka pamoja na kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.

Rais Samia, ametoa tahadhari hiyo leo Jumatano, tarehe 7 Julai 2021, alipozungumza na wananchi wa Kibaigwa, Mkoa wa Dodoma, akiwa safarini kwenda mkoani Morogoro katika ziara ya kikazi ya siku mbili.

“Tuendelee kuchukua tahadhari zote kuhusu corona. Wimbi hili la tatu lipo nchini, tuna wagonjwa Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, maeneo mengine na hata Dodoma kwa kiasi kidogo wapo,” amesema Rais Samia

Tarehe 28 Juni 2021, Rais Samia akizungumza na wahariri na waandishi wa habari, Ikulu ya Dar es Salaam, kuhusu siku 100 za utawala wake, alisema, Tanzania kuna wagonjwa zaidi ya 100 wa corona.

Alisema kati yao, 70 wanaendelea na matibabu katika hospitali ambazo hakuzitaja wakiwa wamewekewa mitungi ya gesi, ili kuwasaidia kupumua.

error: Content is protected !!