May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais wa Haiti auawa katika shambulio

Spread the love

 

JOVENEL Moise (53), Rais wa Haiti ameuawa leo Jumatano, tarehe 7 Julai 2021, katika shambulio akiwa katika makazi yake. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Pia, katika shambulizi hilo, imeripotiwa Martine Moise, mke wa rais huyo, amejeruhiwa na amelazwa hospitalini.

Kaimu waziri mkuu wa nchi hiyo amesema, hatua zote zinachukuliwa “ili kuhakikisha serikali inaendelea.”

Moïse, amekuwa madarakani tangu Februari 2017, baada ya mtangulizi wake, Michel Martelly kung’atuka mamlakani.

Katika kipindi hicho cha utawala wake, Moise alikuwa akikabiliwa na tuhuma za ufisadi hali iliyosababisha maandamano ya mara kwa mara ya wananchi wa kupinga uongozi wake.

Katika maandamano ya mwaka 2019 ya kumpinga, Rais Moise, alisema “hatondoka nchini kwasababu ya shinikizo kutoka kwa magenge yaliyojihami na walanguzi wa dawa za kulevya.”

Mapema mwaka 2021, maandamano yalifanyika yakimtaka kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na tuhuma mbalimbali.

error: Content is protected !!