Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa avutiwa na mchango wa NBC kuchochea kasi ya kilimo, biashara na michezo
Habari Mchanganyiko

Majaliwa avutiwa na mchango wa NBC kuchochea kasi ya kilimo, biashara na michezo

Spread the love

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameonyesha kuvutiwa na mchango unaoendelea kutolewa na benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika kukuza sekta mbalimbali nchini ikiwemo kilimo, biashara na michezo kupitia huduma na ufadhili wa benki hiyo kwenye maeneo hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viunga vya ukumbi wa Mkutano Mkuu wa saba  wa mwaka wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika Mkoani Lindi. Benki ya NBC ni moja ya wadhamini muhimu wa Mkutano huo wa siku mbili.

Akiwa kwenye banda hilo Waziri Mkuu alipata wasaa wa kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo katika sekta mbalimbali ambapo alionyesha kuvutiwa na huduma ya NBC Shambani inayotolewa na benki hiyo mahususi kwa wakulima wakiwemo wakulima wa zao la korosho.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akitazama baadhi ya vipeperushi kuhusu huduma  zinazotolewa na Benki ya NBC huku akimsikiliza Meneja wa NBC tawi la Lindi, Iovin Mapunda (Kushoto) akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo akaunti ya NBC Shambani mahususi kwa wakulima wakati Waziri mkuu alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viunga vya ukumbi wa Mkutano Mkuu wa saba  wa mwaka wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika Mkoani Lindi. Benki ya NBC ni moja ya wadhamini muhimu wa Mkutano huo wa siku mbili.

Waziri Mkuu Majaliwa pia aliipongeza benki hiyo kwa mchango wake kwenye sekta ya michezo hususani udhamini wake kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara yaani NBC Premiere League, Ligi ya Vijana pamoja na NBC Championship.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kesi ya mfanyakazi wa CRDB itaendelea J’tatu

Spread the love  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam inatarajia...

Habari Mchanganyiko

Mawasiliano Dar – Bagamoyo yarejea

Spread the loveMAWASILIANO ya barabara ya Mkoa wa Pwani na Dar es...

Habari Mchanganyiko

Tanesco: Mvua chanzo kukatika umeme leo

Spread the loveShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limedai kuwa hitilafu iliyojitokeza katika...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Zara tours yajivunia kupandisha wageni 228 Mlima Kilimanjaro

Spread the loveKampuni ya utalii ya Zara tours ya mjini Moshi mkoani...

error: Content is protected !!