Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa atamani Mulugo ahamie Lindi
Habari za Siasa

Majaliwa atamani Mulugo ahamie Lindi

Mbunge wa jimbo Songwe, Philipo Mulugo
Spread the love

 

KUTOKANA na kupungua kwa kero zilizokuwa zikiwakumba wananchi wa Jimbo la Songwe mkoani hapa, Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Mbunge wao, Philipo Mulugo ili maendeleo yazidi zaidi kupatikana. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe… (endelea).

Majaliwa aliyasema hayo jana tarehe 16 Februari 2023 katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Songwe.

Alisema wilaya ya Songwe ni moja ya wilaya mpya nchini ambayo kimuundo ni ya mwisho lakini serikali imepeleka fedha nyingi zilizotumika kujenga miradi inayogusa jamii huku ikielezwa kuwa changamoto kubwa katika jimbo hjilo ni ujenzi wa barabara kuu kutoka Mbalizi hadi mkwajuni.

‘’Nimeona mabadiliko makubwa ya ujenzi wa miradi iliyojengwa kwa fedha za serikali kuu na mingine imejengwa kwa fedha za ndani, nimeshangaa leo Mbunge anaitwa (Papaa Mukulu) ningependa Mulugo ahamia Lindi akapige kazi huko, maendeleo na utulivu uliopo hapa umenikosha’’ alisema Majaliwa.

Alisema kulikuwepo na migogoro kati ya Mbunge na mkuu wa wilaya lakini sasa hakuna tena.

Alisema ameikagua barabara iliyojengwa na Tarura ambayo iliahidiwa na Rais wa awamu ya tano Hayati Dk. John Magufuli na kuridhishwa na utekelezaji wake.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo, Philipo Mulugo, alisema barabara hiyo iliahidiwa wakati wa utawala wa awamu ya tano lakini imejengwa na kukamilika awamu ya sita sambamba na miradi ya maji, afya, umeme na mimgineyo inaendelea kujengwa.

Alisema barabara kuu kutoka Mbalizi hadi makao makuu ya wilaya ya Songwe – Mkwajuni imepigiwa kelele Bungeni kila mwaka hivyo alimuomba waziri mkuu kutoa majibu ya serikali mbele ya wananchi kueleza mchakato ya utengenezaji barabara hiyo inayosubiriwa kwa hamu pamoja na ujenzi wa madaraja kuunganisha kata kwa kata.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Aidha, Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Godfrey Kasekenya alimtoa hofu Mbunge Mulugo akimueleza upembuzi yakinifu umefanyika hivyo kipindi kijacho ujenzi utaanza pamoja na madaraja.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara kilomneta moja meneja wa Wakala wa barabara vijijini (TARURA) wilayani humo,Yusuph Shabani,alisema ujenzi wa barabara hiyo ya kiwango cha lami kilometa moja ulianza tarehe 10 Agosti 2021 na kukamilika tarehe 10 Aprili 2022,kwa gharama ya Sh milioni 500 za mfuko wa jimbo.

1 Comment

  • KAMA BADO ANA AMINI UTI WA MGONGO NI ELIMU KWENYE LIKE JICHO TUWEKE LIKE FATHER LIKE SON (HASA KWENYE KIFO CHAO) MAANA NILILIDHI NGOMBE NA UJUZI WA KUCHUNGA NGOMBE KUTOKA KWA BABU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!