WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo tarehe 15 Julai, 2022 ameanza ziara ya kikazi mkoani Singida na kutembelea mradi wa ujenzi wa shule itakayonufaisha wanafunzi zaidi ya 600. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).
Majaliwa ameanza kwa kutembelea Shule hiyo ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Singida iliyopo katika kata ya Solya, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Ujenzi wa Shule hiyo ambao unatekelezwa kwa awamu mbili, utagharimu shilingi bilioni 4 mpaka kukamilika kwake.
Halmashauri hiyo ilipokea shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kugharamia ujenzi katika awamu ya kwanza.
Mradi hui utakapokamilika utawezesha wanafunzi 600 kutoka mkoa wa Singida kupata fursa ya elimu ya Sekondari.
Leave a comment