October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama kuu yaagiza wadeni watatu wa Exim kukamatwa kwa kushindwa kulipa deni la Sh milioni 674

Spread the love
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania (Idara ya Biashara) jijini Dar es Salaam
imeagiza kukamatwa kwa wadeni watatu wa benki ya Exim Tanzania kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya kulipa deni lenye thamani ya  Tsh 674.4m / – na zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 2. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Kwa mujibu wa hati ya kukamatwa kwa wadeni hao iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi ya kibiashara nambari 95 ya mwaka 2015,  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Justine Masejo ameagizwa kuwakamata wadeni hao watatu ambao ni Chimanbhai Marghabai Patel, Pratik Chimanbhai Patel na Sonia Pratik Patel.
Kwa mujibu wa Hati hiyo iliyosainiwa mnamo Septemba 13, 2021 na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, inasema watatu hao walihukumiwa katika kesi hiyo
tarehe 16 Septemba, 2016, kuilipa Benki ya Exim Tanzania Limited kiasi cha fedha Tsh
674,440,547.55 na Dola za Kimarekani 2,024,094.14 pamoja na riba na gharama
ya kesi hiyo.
Hata hivyo Iicha ya hukumu hiyo kutolewa, pesa hizo bado hazijalipwa kwa benki hiyo.
Aidha, ni kufuatia ucheleweshaji huo, ndipo mahakama hiyo iliamuru kukamatwa kwa watatu hao isipokuwa tu iwapo wangelipa deni hilo na kuongeza kuwa
watatu hao wangepaswa kufikishwa mahakamani haraka iwezekenavyo.
“Unaagizwa kurudisha hati hii mnamo tarehe 27 Oktoba,
2021, sambamba na uthibitisho unaoonesha siku na namna
ambavyo hati hii imetekelezwa au sababu zilizosababisha kushindwa kutekelezwa kwake.” ilisomeka sehemu ya hati hiyo.
error: Content is protected !!